Wasanii uongo uongo unakwamisha endelezo la sanaa ya muziki.

Wasanii uongo uongo unakwamisha endelezo la sanaa ya muziki.

Mswahili hunena yakuwa “Afadhali kuwa na jirani mchawi, kuliko muongo” hakika ni semi kuu yenye maana kwa mwenye tafakari.

Uongo unaharibu mengi mno, ingawa wenyewe wenye kupenda uongo hunena eti! ‘unajibrand’.

Kimsingi kutengeneza chapa yako si lazima kunena semi nyingi za uongo, bali kweli yenye kweli yenye uhalisia wake.

Uongo ndiyo unafanya sanaa ya muziki ishindwe kusonga kwa haraka, na uwazi ni kwamba wanachopata wasanii sicho ambacho wanaaminisha wengi katika mengi.

Muziki bado uko vibaya hakuna gawio la faida kubwa ambayo wasanii wengi wanaaminisha mashabiki wa muziki.

Ni kawaida kabisa msanii kunena hadharani yakuwa na miliki hiki na kile na huku picha za ufahari zikitawala katika mitandao, ilihali uhalisi wa maisha yake sio ule.

Na mwisho wa siku hata akipata changamoto ya mengi ya kimaisha basi hutaka tena jamii imchangie kwa mapana katika utatuzi wa changamoto hiyo/hizo. (Soni)

Lakini ukitafakari kwa mapana yale maisha ambayo alikuwa anatuonyesha yunayo hakika huwezi fikiria kama atahitaji changio katika mengi, bali yeye kuwa mhamishaji wa kuchangia mengi katika jamii.

Yapasa wawe wazi katika uwazi wa uhalisi ili hata wale viongozi ambao hupiga nao picha na glasi za juisi wajue sanaa bado ni mkwamo wa kipato.

Uongo unafanya hata wao viongozi waone sanaa iko vyema mno katika pato, ila uhalisi wenye uhalisia wasanii wetu ni masikini wenye majina makubwa.

Na ikumbukwe tunapozungumza swala la maendeleo ya sanaa (Faida) hatupaswi kutazama mtu mmoja bali mapana ya wote kwa uwingi.

Ni vyema wasanii msimame katika kweli yenye kweli maana “Kweli itakuweka huru” lakini “Kweli ndiyo fimbo ya kukamata”

#TuzungumzeMuziki