Wasanii ni lini mtajifunza kwa Diamond Platnumz?

Wasanii ni lini mtajifunza kwa Diamond Platnumz?

“Amepata fimbo,amepata mambo” kwa hakika  msemo huu wa waswahili  unaishi vyema kwenye maisha ya Sanaa ya Diamond Platnumz.

Ni vyema upatapo nafasi uitumie vyema tena kwa 100% kwa maana wakati wote muda haurudi nyuma, lakini waswahili husema “Bahati haiji mara mbili”.

Ila hata Fid Q aliwahi kusema “Thamini huu muda kabla haujageuka histori”. Ni wazi kwa upana bila kuuma maneno Diamond ni mtu wa kutumia muda vyema kwa maana nyakati zote akikutana na msanii mkubwa huwa haishii kupiga picha tu bali kazi yenye kuleta mafanikio katika maisha yake ya Sanaa na nje ya Sanaa.

Tumeona jana video zikisambaa Diamond akiwa na Omarion ikiwaonyesha wakifanya video ya wimbo. Jambo hili ni kubwa na zuri kwa maana ya kuzidi kujiongezea wigo wa kufahamika Zaidi lakini kuwa msanii mwenye ushirikiano Zaidi na wasanii wengi wa nje.

Nafasi za kukutana na wasanii wakubwa kwa upande wa wasanii wetu huzipata wasanii wengi, ila wengi wao wamekuwa wakiishia kupiga picha na kuweka mtandaoni huku kukiwa hakuna cha kuendelea chenye kuleta maana Zaidi.

Hivyo kuna wakati yapasa tujifunze vyema kwa yule ambaye amefanikiwa, kwa maana tukiwa na kina Diamond wengi ni wazi muziki wetu utakuwa ni wenye faida Zaidi.

Hivyo kujifunza yaliyomema yenye maana ya mafanikio ni jambo jema wakati wote.

#TuzungumzeMuziki.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa