Wasanii msijipe matumaini juu ya mdau, amali yake haina mwisho, wala macho yake hayashibi utajiri.

Wasanii msijipe matumaini juu ya mdau, amali yake haina mwisho, wala macho yake hayashibi utajiri.

Nani amfunge paka kengere? ilihali kila mmoja anaepusha vyema kichwa chake lakini pembezoni kutoa lawama nyingi juu ya mfumo kandamizi kwa wasanii kutoka kwa mdau.

Furaha ya mdau ni yeye kuendelea kujiweka sawa kimaisha lakini hana maana mbele ya maisha ya wasanii wengi kwa maana ya wakati wote kuwatumia vyema bure.

Lakini ndugu zetu wasanii yapasa mjue ni afadhari muwe wawili kuliko mmoja, kwa maana mkiwa wawili mmoja akianguka basi mmoja atamuinua mwenzake, hapa tunalenga umoja maana umoja ni nguvu.

Lakini Roma aliwahi kusema “Mdau anachenga nyingi kama alichezea Tukuyu”

Maana ni wazi mdau anajua vyema namna ya kucheza na akili za wasanii wengi katika kuwaweka makundi mawili na bila umakini makundi haya hayawezi kuunganika lakini hapo ndipo njia njema ya mdau katika kuweka sawa upana wa utawala wake juu ya Sanaa.

Jambo baya na lakushangaza mpaka leo hii ni wasanii wengi kuendelea kutumika vyema bure bila mdau kujali wasanii nao wanafamilia ambazo zinahitaji msaada kutoka kwa msanii husika.

Ila mdau amevijika upofu na kuendeleza mfumo kandamizi juu ya wasanii wengi mno, jambo hili si jema katika uhalisia ila ni jema kwa mdau maana anatimiza malengo yake kupita jasho jepesi la wasanii wengi ambao wamezingirwa na uonyoge katika mioyo yao ila furaha ya uongo katika nyuso zao.

Ni wazi majina ya wasanii hayafanani hata kwa udogo na kazi wafanyazo, wakati mdau akimtumia vyema msanii katika matamasha yake ni wazi yeye anafaidika na mdhamini tamasha lakini hata viingilio vya matamasha.

Lakini bado mdau anataka vyote achukue yeye na msanii hana kauli maana huogopa kuzimiwa kabisa kupigwa kwa nyimbo zake lakini hata kukosa yote kuanzia ngazi ya matangazo ya makampuni.

Maana wanasema muziki umekua lakini sisi hatuamini katika hilo kwa maana upana wa udalali wa mdau juu ya kampuni kumfikia msanii ni mkubwa mno.

 

Itaendeleaa…..

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa