Wasanii mmejifunza nini kwa Vanessa Mdee na Jux

Wasanii mmejifunza nini kwa Vanessa Mdee na Jux?.

Tunaona namna ambavyo wasanii wamekuwa ni wepesi mno katika kutoa pongezi kwa Vanessa na Jux katika tamasha lao la Ilam.

Tamasha hili limeenda mikoa 5 ambapo kila mkoa waliweza kufanya tumbuizo wakiwa na wasanii wengine wengi.

Na katika uhalisi Vanessa Mdee na Jux ni wasanii wapya katika uzao wa muziki wa kizazi kipya, hapa tukiwa na maana ni kizazi cha pili katika muziki huu.

Lakini wameweza kufanya jambo kubwa mno ambapo wapo wasanii wengi wenye ujazo wa kutosha na hawakuwahi kuwa na uthubutu katika ufanyaji wa matamasha yao bali kusubiri simu ya promota.

Hivyo wasanii katika pongezi nyingi mtoazo kwa Vanessa Mdee na Jux, je! mmejifunza nini?.

Ni vyema hawa wawe somo katika ukamilisho wa neno muziki umekua sasa, ni vyema wasanii wengi mkawa na matamasha yenu binafsi hii itazidi kuongeza thamani ya muziki wako/wenu.

Msiishie katika pongezo tu bali kiwe kitabu cha kusoma na kuelewa kuanza vyema katika leo zenu za sanaa zenu.

Tizneez tunawapa pongezi Vanessa na Jux katika tamasha lenu llam hakika mmefanya sawia kwa usawa wenu.

Tegemeo letu ni kuongeza idadi ya mikoa katika nyakati zijazo, tunaamini itakuwa hivyo kwa upana wenu.

#TuzungumzeMuziki