Wasanii kwenye sanaa ya muziki wala hawapo hivi, bali huo upande mwingine. (Soni

Wasanii kwenye sanaa ya muziki wala hawapo hivi, bali huo upande mwingine. (Soni)

Hii sanaa ambayo leo hii imeonekana kuwa rahisi ilikuwa ni ngumu mno hapo awali katika kuchonga njia na kufika leo hii. (Nidhamu)

Na njia katika kuchonga ni upana wa ushirikiano wa Dj na msanii kwa upamoja mkuu. (Muda)

Leo msanii kumtolea maneno yenye fedheha Dj hakika ni kitu kibaya zaidi. Na kadri siku zinavyoenda wimbi la wahuni katika uvamizi wa sanaa ya muziki ni wazi italeta anguko katika mengi. (Hakika)

Tafakari kitendo hiki ni mbele ya wengi katika Miss Kinondoni, ambapo Amber Lulu ni msanii alikwa katika toa burudani. (Eeh)

Na burudani yake ikajaa soni kuu katika lugha kali kwa Dj lakini kwa wageni wengine waalikwa. (Soni)

Je! matendo ya namna hii yanakuza sanaa? ni wazi yanaleta anguko. Na hapa watu hawafikiri katika upana wa msanii bali wasanii. (Kabisa)

Wasanii wengine hawapo hivyo bali huyu katika mengi yake yenye fedheha kuu. Ikumbukwe muziki huu wasanii wengi wenye upana wa kujua biashara wamepambania mno. (Nyakati)

Na video hii inaonyesha yakuwa Amber Lulu hakuwa sawa kichwani mwake huenda alitia kileo. Na kiasi cha kusahau alienda pale kama nani. (Fedheha)

Kama angetoa burudani kuu hakika hata mwakani huenda angepata shoo nyingine kupitia Miss Kinondoni. (Eeh)

Lakini pia kupitia onesho lile huenda wadau wengine wengeona ubora wake na kupata mialiko mingi zaidi baada ya pale. (Naam)

Lakini alichofanya ni fedheha kuu ambayo mwenye utashi kamili hawezi kutazama juu ya mualiko wa Amber Lulu bali kumpuuza vyema. (Uhalisia)

Lakini pia kuna kila sababu ya wadau kupuuza wasanii wa aina hii. Na ifike mahala Dj apewe heshima yake katika ukuu. (Pande Zote)

Na shangazo kuu kwa wasanii aina ya Amber Lulu waliojaa hovyo hutenda hovyo kisha kimbilio huwa mtandao wa picha ‘Instagram’ kujiombesha radhi. (Shangazo)

Hii haitushangazi washamba sisi kwa maana twajua lengo ni mzunguko wa mtandao, lakini kwa upana ni kuharibu biashara ya muziki kabisa, bali tamba ya hovyo. (Ujinga)

Yote ya yote twajua yakuwa “Kinywa cha mjinga, hunena ujinga” (Daima)

#MuzikiNiSisi