Wasanii kupigwa radioni 90% sio mwisho wa matatizo.

music

Wasanii kupigwa radioni 90% sio mwisho wa matatizo.

Juhudi za wasiojiweza, ni moja kati ya nyimbo zangu chache ambazo huzisikiliza mara nyingi kwa siku. Wimbo huu ni wimbo wa msanii Fid Q ambapo ameshirikisha Bi kidude, ambaye sasa ni marehemu.

Hakika wimbo huu wa juhudi za wasiojiweza ni wimbo unaendana na maisha halisi ya wasanii wetu wa muziki kwa kizazi kipya katika kila pande ya maisha yao. Ni wazi Fid q ni mwenye maono maana ameliona hili miaka 4 nyuma.

Ni wiki kadhaa zimepita tangu kuona kampeni za wasanii walio wengi wa muziki wa kizazi kipya, ambapo kampeni hii ilihusisha zaidi mtandao wa picha “Instagram”

Kampeni hii imetaka wasanii kutaka kupigwa zaidi muziki wao kwa 90% katika vyombo vya habari hapa nyumbani Tanzania

Sina hakika kama kweli vyombo vya habari sasa hazipigi 90% ya nyimbo za nyumbani, maana ni wazi vipindi vingi vinaendeshwa na muziki wa kizazi kipya. Isipokuwa lawama za kupendelewa kirafiki, kimkoa, na rushwa zimekuwa kubwa zaidi. Ila ni wazi wasanii walio wengi huwa hawasemi zaidi ya kulalama pembeni.

“Kama haujutii ya jana hakika hauta hofia ya kesho”msemo huu naufananisha kabisa na maisha ya wasanii wetu wa muziki wa kizazi kipya, ambao wamekuwa vinara wa kupigania hili na hata kulalamika kila iitwapo leo katika mambo mengi yanayoendelea kwenye muziki. Inamaana mara hii wameshasahau madai waliokuwa wakipigania miezi kadhaa nyuma?

Naitazama hoja hii kwa mapana zaidi, kama vyombo vya habari vitacheza nyimbo kwa 90% hakika tupata kuwafahamu kama ilivyo sasa. Ila ni wazi madai ya kupigwa zaidi si hoja ya kutumia nguvu walioitumia zaidi, isipokuwa walipaswa kufikiria malipo yapo kuanzia ngazi ya mirabaha, matumbuizo, na hata katika kampuni za simu ambazo hutumia nyimbo zao.

Wasanii walio wengi ni wasanii wenye hofu katika kuonyesha ukweli kama sio kueleza katika mahojiano yao. Nadhani hawajui “Hofu haina msaada zaidi ya kukupunguzia akili”

“ Mfa maji haishi kutapatapa” ni miezi kadhaa tumeona wasanii hawa hawa walibuka na hoja nyingi ambazo walitaka serikali iweze kuwapa msaada. Lakini moja ya mengi yaliongelewa ilikuwa ni la malipo ya mirabaha ambayo ni wazi ilitangazwa na Mh Nape kuanzia tarehe 1/1/2016 wataanza kupokea malipo hayo. Lakini mpaka sasa hakuna msanii aliyesema kama amepokea, isipokuwa naona   makundi mawili ya wasanii, wanaotaka kulipwa na wasiotaka kulipwa.

Hii inanifanya nione wazi kuwa wasanii wetu ni wafa maji maana ni watu wa kutapatapa maana kabla hili halijakamilika wanataka hili. Na hakika kabla la hili litaibuka jingine na hili la 90% wataliacha kama lilivyo.

“Wapo wenye hisia juu wadau kutumia akili ya kuwapa hoja nyingi baadhi ya wasanii ili kuvuruga mambo mengi ambayo yatawapa manufaa makubwa katika kazi zao. Maana wadau si watu wakupenda msanii awe na nguvu zaidi kuliko wao.”

Ingawa daima huwa sipendi kutumia hisia bali ushahidi kamili katika hoja kama hizi zenye kujenga.

“Mtaka yote kwa pupa hukosa yote”

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez