Wasanii chipukizi tangulizeni kazi mbele si rushwa.

Wasanii chipukizi tangulizeni kazi mbele si rushwa.

Ni kawaida kuona jumbe za wasanii wengi chipukizi katika kuomba mahojiano ama kucheza wimbo wake kwenye ‘Media’.

Chukizo ni katika kutanguliza rushwa mbele kuliko kazi yake, jambo hili haliko sawa. Lakini chanzo kikuu ni madj wengi katika ‘Media’ kuweka mbele zaidi mkono wa kupokea rushwa kuliko kazi ya msanii.

Jambo hili linafanya wasanii chipukizi kuona yakuwa huhitajiki kufanya kazi bora katika kusikika bali namna ya mkono kuwa mrefu na mwepesi katika utoaji wa rushwa.

Maana aliyetoa rushwa ndiye ambaye atasikika kwa upana hata kama wimbo wake hauna ubora wowote ule, ila asiyetoa na wimbo wake ni bora hakika hana nafasi.

Jambo hili ni baya mno kwa upande wa Madj wengi zaidi, maana katika uwazi linafanya tukose kazi nzuri toka kwa wasanii chipukizi bali vilai visivyo na maana.

Ingawaje yapasa wasanii chipukizi watangulize kazi mbele si rushwa licha ya uhalisi wa uhalisia wa sasa ni kutazama rushwa si kazi bora kwa madj.

Lakini pia pesa ambayo amekuwa akiomba dj ni vyema utumie katika kutangaza kazi yako kwa upana katika mitandao ya kijamii.

Lakini ndugu zetu madj tunawakumbusha hata neno kuu la lanena “Toshekeni na mishahara yenu”

Chezeni wimbo kulingana na ubora si kwa upana wa rushwa, uhalisi tukicheza kazi zilizo bora tunazidi kusogeza muziki wetu mbele zaidi.

Pongezi kwa Madj ambao wao hawachukui rushwa na kusimamia kazi ya msanii yenye ubora katika kuicheza kwenye kipindi.

#TuzungumzeMuziki