Wasanii 10 bora wa hiphop wenye kila sababu ya kupewa nafasi na Media.

Wasanii 10 bora wa hiphop wenye kila sababu ya kupewa nafasi na Media.

Team Tizneez tunaandika aina zote za muziki kwa maana ya muziki wa kizazi kipya lakini tumekuwa ni wahudhuliaji wazuri katika majukwaa mengi ambayo yanahusisha muziki wa hiphop.

Kumekuwa na vilinge vingi vya hiphop kuanzia kile cha Kilingeni cha pale msasani ambacho hiki ni chachu cha vyote ambavyo vimefuata lakini kilinge hiki kimeweza kuwa na nguvu ya kutoa vijana wengi katika muziki wa hiphop lakini kilinge kile ni darasa kubwa kwa maana ya wengi ambao wanafanya katika vilinge vingine ni uzao halali wa Kilinge cha Msasani.(Wasanii)

Sasa hivi kuna Kinasa cha Maalim Nash ambacho hufanyika Temeke uwanja wa shule ya msingi Madenge. Lakini Kinasa kinatoa nafasi ya wasanii wa aina zote kutumia jukwaa hilo kuonyesha kipaji ulichonacho/alichonacho.

Open Mic Thursday Ni jukwaa la msanii Fid Q ambalo sasa hufanyika  Micasa Tabata kila siku ya alhamisi ambapo na chenyewe hutoa nafasi kwa wasanii wote kuonyesha Sanaa zao walizonazo.

Ila majukwaa yote haya wasanii ambao hujitokeza kwa wingi ni wasanii wa hiphop.

Team Tizneez tumeamua kuandika listi ya wasanii 10 ambao ni wazi uwezo wao katika majukwaa haya umekuwa ni mkubwa, lakini hata uwezo wa kazi zao katika nje ya majukwaa haya ni mkubwa.

Katika listi hii tumezingatia mambo matano tu ambayo ni Uandishi, midondoko, kutawala jukwaa, kujiamini, na nidhamu.

Hivyo namba moja ni  I.Maaarifa Big Thinker

2.Dizasta Vina

  1. Black Fire
  2. Sele Mentali
  3. Mo Rymes
  4. Logic Jerry
  5. Boshoo Ze Son

8.H 255

9.Wakiafrica

  1. Mtashi Balaa.

Wapo ambao wanaweza kushangaa kwanini hatujamuandika Bassalt lakini ni wazi nidhamu yake ipo chini mno, hivyo hawezi kuingia katika listi hii kwa maana amekosa kigezo kimoja.

Ni wazi hao wanahitaji nguvu ya media kubwa ili waweze kuonyesha uwezo wao kwa watanzania wapenzi wa hiphop.

#TuzungumzeMuziki

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Tuachie maoni yako hapa