Wapendwa watayarishaji wapya wa muziki yapasa mjue wasanii hawana soni baada ya kuwatumia.

Wapendwa watayarishaji wapya wa muziki yapasa mjue wasanii hawana soni baada ya kuwatumia.

Kwa hakika kilio cha watayarishaji wengi kuhusu mafanikio kwa kazi kubwa waifanyayo ya muziki ni kubwa mno.

Wapo ambao walistuka lakini nyakati zao zilishapita hivyo wakabaki na historia yakuwa niliwahi fanya hiki na kile au wimbo huu na huu ilihali mifuko ikiwa imetoboka lakini msanii akiwa amesheheni mafanikio.

Jambo hili baya mno kwa upande wa watayarishaji maana tunaendelea kuona ya namna ambavyo wakiwa chanzo cha mafanikio makubwa ya wasanii ilihali wao kuwa hoehae.

Tumeona mwaka 2016 mpaka 2018 kumeibuka kwa watayarishaji wengi mno. Na pia katika miaka hii/hiyo tumeona namna ambavyo wasanii wengi wakihama hama studio lakini wengi kuhama mara tu mtayarishaji akitaka malipo.

Watayarishaji wakongwe kama Hermy B, Majani, Master Jay, Man Water, na wengine wengi si watu wa kutaka kufanya kazi bure bali kutambua thamani yao na haki zao.

Hivyo unaona kwa namna ambapo uchache wa kutoa nyimbo imekuwa ndogo mno maana wasanii wenye utayari kulipa ni wachache.

Lakini watayarishaji wapya wameweza kutoa nyimbo nyingi mno katika mwaka 2016 mpaka 2018.

Lakini ukitoa msanii kumposti Instagram je!mtayarishaji amepata malipo stahiki?

Lakini watayarishaji hawa wameonekana kufurahia maisha ya kupostiwa Zaidi katika mtandao wa picha huku wakipewa Zaidi sifa lakini katika uhalisia hawaishi katika usawa wa kazi wafanyavyo.

Ila tunapenda tuwakumbushe yakuwa wasanii hawa ambao huwasifu Zaidi mtandaoni ni wasanii ambao hawana soni mara baada ya kuwatumia na kuweza kupata mafanikio yao kama wasanii.

Hivyo kuamka kifikra ni jambo ambalo wanapaswa sasa kuwa nalo maana waswahili husema “Nyakati hupita kiwepesi kama upepo”.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa