Wanaokosoa wimbo wa Picha wa Zaiid hawajui maana ya sanaa ya muziki.

Wanaokosoa wimbo wa Picha wa Zaiid hawajui maana ya sanaa ya muziki.

Shangazo kuu ni namna ya watu waliojivika ushabiki na uchambuzi wa hiphop kukosoa kwa upana wimbo wa ‘Picha’ wa Zaiid.

Na wengine huenda mbali kwa kutoa lugha kali kwa gadhabu kubwa kwa maana ya kuona Zaiid amekiuka misingi. (Fedheha)

Ila haishangazi gadhabu zao wala lugha zao kali, maana hata mswahili hunena yakuwa “Mpumbavu asipoelewa jambo hugadhibika bali mwerevu hukuna kichwa”

Jambo jema ambalo tunapenda kumpongeza Zaiid ni kujua yakuwa ‘Biashara ni uwekezaji’ “lakini ‘Jinsi na kuwa’ katika ufanyaji wa biashara ya muziki.

Biashara ya muziki inahitaji wateja wapya (Mashabiki) kila leo, sasa utawezaje kupata wateja wapya kama utabaki katika ladha moja kila iitwapo siku? hakika haiwezekani.

Lakini inapaswa ikumbukwe yakuwa msanii anaweza kufanya lolote lile katika sanaa ya muziki, kikubwa ni kuwa na uwezo na kufanya kwa ubora wa juu.

Je! wimbo wa Picha wa Zaiid amefanya katika kiwango kipi? kwa uhakika twanena yakuwa ni kiwango cha juu.

Na tukumbuke yakuwa Sanaa ya muziki “Ni ufundi ambao anatumia msanii ili kuwasilisha fikra/mawazo yaliyoko ndani yake, vilevile Sanaa ya muziki ni uzuri unaojibua katika umbo lililosanifiwa.

Ilihali kusanifu ni kuumba au kufanya jambo au kitu kwa kutumia ustadi ili kiweze kuvutia kwa hadhira.

Msanii hueleza hisia zake katika upana wa Sanaa ya muziki, na katika uhalisi yaweza kuwa kwa ala za muziki au bila hata ala za muziki.

Kwa upana huo wa sanaa ya muziki, yupo ambaye anasababu ya kukosoa wimbo wa Picha?

Hakika hayupo basi tuendelee kuburudika wimbo huu, maana upo katika ubora wa maana na wimbo kamili.
#TuzungumzeMuziki