Wakati muziki unaendelea mbele wapo mashabiki wengi wanaurudisha nyuma.

Wakati muziki unaendelea mbele wapo mashabiki wengi wanaurudisha nyuma.

Ni vyema kuisema ile kweli yenye kujenga muziki katika muendelezo mwema kwa maana ya wasanii wetu kuishi angalau kwa usawa na nguvu yao ya ubunifu wa kazi zao.

Ni wazi Team Tizneez tupo katika makundi mengi ya WhatsApp na tunaona nguvu watumiayo mashabiki wengi kutumiana nyimbo za wasanii wengi.

Na nyimbo hizo hutumiana mara baada ya msanii kutoa wimbo huo katika ngazi ya mtandao. Katika kutumiana WhatsApp ni wazi msanii husika hana faida apatayo juu ya shabiki kumtumia shabiki mwenzake wimbo.

Ni vyema mno shabiki kutuma link mtu aweze kupakua mwenyewe, kwa maana kupitia kupakua nyimbo kwenye ngazi ya mtandao ni wazi msanii husika atafaidika na kuongeza kipato.

Ni wazi nguvu ya kutuma nyimbo WhatsApp inarudisha nyuma muziki na maendeleo ya muziki kwa ujumla. Maana kama mashabiki wote watakuwa wananunua kazi za msanii kwenye mtandao ni wazi muziki utaendelea kukua na kumpa faida kubwa msanii na kuona uboreshwaji mkubwa wa kazi za wasanii wetu.

Shabiki wa kweli wa msanii husika na muziki kwa ujumla ni wazi atahakikisha msanii wake anafaidika na kazi yake ya Sanaa.

Kama wewe ni shabiki wa kweli hakika huwezi kutuma nyimbo WhatsApp bali kupakua mtandaoni ili msanii aendelee kufanikiwa na kufanya kazi bora.

Shabiki sema #MimiSitumiWimboWhatsApp Msanii sema #ShabikiUsitumeWimboWhatsApp #TumaLinkWhatsApp

#TuzungumzeMuziki.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa