Wajuzi wanampinga, hadhira inamkubali Nay wa Mitego.

Wajuzi wanampinga, hadhira inamkubali Nay wa Mitego.

Ni wazi kwa wajuzi wa utamaduni wa hiphop hawajawahi kumuelewa na humpinga Nay wa Mitego katika utamaduni huo. Na nyakati zote hunena yakuwa ni rapa mwepesi ambaye hana uwezo wa uandishi lakini midondoko pia.

Na wajuzi hufika mbali kiasi cha kunena yakuwa “Usimtaje Nay kama msanii au muumini wa utamaduni wa hiphop” ‘Hafai’.

Mitazamo hiyo ya wajuzi haina nguvu mbele ya hadhira ya wengi ambayo yenyewe haina ujuzi mpana juu ya hiphop, isipokuwa kujua uhalisi wa wimbo katika nyakati.

Nay ni mjanja katika kucheza na uhalisi wa matukio katika kweli, na huinena kweli yenye kweli bila woga na jamii kupokea kweli hiyo kwa mapana yake.

Wapo ni moja ya wimbo wake ambao kila mmoja alifurahishwa na kweli ile. Hivyo inaonyesha yakuwa hadhira inapenda uhalisi na si kusimama katika upana na ujuzi wa hiphop.

Lakini wapo ambao hawaachi kuwauliza wajuzi yakuwa “Kama hiphop ni muziki wa ukombozi na ukweli, mbona wasanii wao hawafanyi kwa upana na uwazi kama Nay?.

Sasa kwanini sisi tusimsifu Nay wa Mitego kama mwana hiphop kwa kuishi uhalisi na kwenda na hali halisi? Hadhira nayo yauliza kwa wajuzi. Hizi nyakati kuna mengi yenye uhalisi yenye kugusa jamii, na hakuna msanii aliyesema kwa uwazi.

Na Nay anaweza akafanya lolote na jamii ikaona umuhimu wake katika kutumia sanaa yake ya muziki kuwasemea. Hivyo hadhira inamkubali Nay na kumuona Nay ni msanii bora kabisa wa hiphop kwa kueleza ile kweli yenye kweli ya uwazi, ilihali wajuzi wanampinga.

Ili hadhira ikubali vyema maneno ya wajuzi juu ya wasanii wengine wa hiphop basi kuna haja ya kufanya kwa upana wa hiphop kuwa sauti ya jamii kwa mapana yake.

#TuzungumzeMuziki