“Wagombanapo ng’ombe ziumiazo nyasi” (Madereva na Wasanii)

“Wagombanapo ng’ombe ziumiazo nyasi” (Madereva na Wasanii)

Waswahili husema “Yaingiayo chunguni ni yatufaayo” lakini katika maisha ya muziki hapana.

Sintofahamu ni nyingi juu ya Witnes na Afande Sele juu ya namna ya wimbo wa uzalendo ulivyofanyika. Msanii Witnes ameonyesha hisia zake katika waraka ambao aliandika na kuutuma kwenye group la wasanii la mtandao wa WhatsApp.

Ambapo amemtuhumu vyema msanii Mrisho Mpoto kwa usaliti wa kubadilisha wasanii ambao walikuwepo kwenye wimbo wa kwanza ambao yeye Witnes alishiriki kikamilifu.

Wakati huo tena Mfalme wa Rhymes Afande Sele akieleza wazi chukizo lake/mtazamo juu ya kushiriki kwa Christian Bella kwenye wimbo huo wa uzalendo. Lakini ndugu zetu yafaa mjue

“Mwenye kisu kikali ndiyo hula nyama” Ni wazi kuna makundi mawili ya wasanii katika yote yanaoendelea kwenye mvutano huu wa nyimbo za uzalendo na kampeni kwa ujumla.

Wapo wasanii wenye kujua hali halisi na ambao hawajui hali halisi ambao wao hata ukiwauliza hawajui lolote bali ni wepesi wa kuposti picha kwenye mtandao wa Picha Instangram na kuweka (Location) kwa hakika ni fedheha.

Katika uhalisia lawama zimeenda zaidi kwa Mpoto lakini kwa mbali Fid Q akisimangwa vyema na mashabiki hasa kwenye ukurasa wake wa mtandao wa picha. Na moja ya simango ambalo ameambiwa na mshabiki ni “Mchumia Tumbo” Na Fid Q amelijibu hilo kwa kuandika “Mchumia tumbo baba ako KLMY)

Lakini katika uhalisia hizi zote za nani alaumiwe na nani asilaumiwe ukweli upo kwa wasanii wenyewe ambao waliachwa na ambao walishiriki.(Unafiki).

Nani amfunge pake kengere? kwa hakika hakuna kwa maana kila msanii kuepusha bawa lake juu ya jambo hili ambalo limejaa ukakasi na ubabe.

Lakini wasanii shiriki yapasa wajue “Haifai hata kidogo mmoja kunufaika kwa uzalendo ilihali wengine wanaumia ni wazi huo si uzalendo”

Na kwa hakika tuyaache haya yapite nafikiri ni vyema wasanii kuendelea na muziki, kuliko kutumia muda mwingi kwenye Group lenu la WhatsApp kwa malumbano kwa maana haitabadilisha kitu wala maana halisi ya “Maisha ya muziki yanahitaji unafiki”

Ila katika ile kweli jambo hili lina Ng’ombe wawili wakubwa ambapo wote hawana uzoefu wa kuendesha muziki, bali nguvu waliyonayo. (Vyeo/Madaraka)

Mvutano/ugomvi wao ni wazi waumiao ni wasanii wetu ambao wamejaa uoga na unyoge. Hivyo mashabiki mwapaswa mjue yakuwa “Sasa muziki unaendeshwa na madereva ambao hawana uwezo wa kuendesha vyema hili gari la muziki”

Ila hata yule dereva mkuu hanao uwezo wa kuendesha bali upendeleo. Ni wazi kwa hakika hakuna mwenye unafuu kati ya madereva hawa wapya na dereva mkuu wa zamani.

Na ili yaishe haya yote ni wazi yapasa Chama Cha Muziki Wa Kizazi Kipya (TUMA) kiwe na nguvu lakini yote hayusuyo wasanii yaanzie kwenye chama kwa hakika hakutakuweko kwa malalamiko haya.

Wakati wote waswahili husema “Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu” Na wala haipaswi kuishi katika maneno haya “Kwa mwoga huenda kicheko, kwa shujaa huenda kilio” kwa maana “Wanyonge ndiyo huonyesha makaburi ya mashujaa. Ni vyema wasanii mjitafakari katika haya.

#TuzungumzeMuziki