Vumbi ya Ray Vany si ushindani wa kisanaa bali matangazo. (Eeh)

Vumbi ya Ray Vany si ushindani wa kisanaa bali matangazo. (Eeh)

Tumeupa sikio katika usikivu wimbo wa Vumbi toka kwa Ray Vany. Ambapo ni wazi si wimbo wenye ukubwa katika usikivu bali udogo kabisa wa ubunifu katika muendelezo wa muziki. (Anguko)

Matangazo ni makubwa mno, na ni jambo jema. Lakini wimbo ni wa kawaida mno kuanzia ngazi ya uimbaji kwa maana jinsi ambayo muimbaji ameimba. (Muziki)

Ray Vany mwanzo wake ulikuwa ni katika ufundi mkuu wa utungaji na uimbaji pia. Lakini leo yake ni katika udhaifu wa tungo nyepesi na uimbaji. (Soni)

Kwenye wimbo huu wa Vumbi hakuna ufundi wa uimbaji katika panda shuka za kucheza na sauti katika wimbo. (Ndiyo)

Uimbaji ni katika minyooko ya moja kwa moja mithili ya mtu aelekeapo nyumbani kwake. Hakuna kona za uimbaji katika uzuri na ladha kamili. (Uimbaji)

Ni vyema Ray Vany akajitafakari katika kesho kwa maana aina ya tungo hizi na uimbaji wa namna hii hazina maisha. (Hakika)

Lakini upana wa ushindani katika matangazo amefanikiwa, lakini upana wa wimbo katika ubora ni wazi hapana. (Sikitiko)

Wajuzi wenye kujua upana wa muziki hawaachi kujiuliza hivi tunasikiliza nini katika wimbo? Tungo, uimbaji au mdundo? (Chekesho)

Ni wazi mashabiki wanapaswa kujua tofauti ya wimbo bora na nyimbo zenye kutrend bila ubora. (Matangazo)

Ray Vany ni msanii mzuri na mwenye ujuzi imara wa utunzi na uimbaji hata kuchana pia. Vivyo akitoa kufuata mtiririko wa nyakati hizi hakika atafanya kazi bora zaidi. (Kabisa)

Lakini akifuata kile kilichopo hakika hatuwezi kuona ubora wake bali udhaifu mkuu. Na yote ya yote hata mswahili anena yakuwa “Kilichopo baharini kakingoje ufukoni” (Trend na muda ujao) 

#MuzikiNiSisi