VINEGA HAWAKUMHITAJI DOKTA MWAKA

ni ushindi

VINEGA HAWAKUMHITAJI DOKTA MWAKA

Ni miaka minne na siku 111 imepita tangu kufanyika kwa Tamasha la Burudani kwa Mashabiki. Tamasha hilo lilifanyika Novemba 26, 2011 katika viwanja vya Taasisi ya Ustawi wa Jamii (wengine huita chuo cha ustawi wa Jamii) kilichopo makutano ya Barabara ya Shekilango na Barabara mpya ya Bagamoyo, eneo linalofahamika kama Bamaga kikipakana na ofisi za TBC, Global Publishers (kwa Shigongo), Bongo Records, Tume ya sayansi na Teknolojia na viwanja vya Posta kijitonyama nk.
Tamasha hilo lilikuwa likiongozwa na Vinega ambao walikuwa wakiupa sapoti harakati za Anti Virus kwa wakati huo. Sina hakika kama harakati hizi bado zipo wenye uhakika mtanisaidia katika comments zenu. Kiingilio cha show siku hiyo kilikuwa ni Tsh 5000. Ni nyakati hizo hizo pia kitabu cha Joseph Mbilinyi kiitwacho SUGU: The Autobiograh, Muziki na Maisha kilikuwa kina siku chache tangu kilipoanza kuuzwa.
Kilichonifanya nishindwe kuikosa hiyo shoo kwanza kabisa sikuwa na sababu ya msingi ya kutokuhudhuria.Pili nyakati hizo sehemu ambayo shoo hiyo ilipangwa kufanyika ndipo nilipokuwa nikichukua mafunzo yangu ya Shahada ya Kwanza. Hamasa kubwa niliyokuwa nayo ni kutaka kuona muitikio wa mashabiki kwa wasanii ambao kama ambavyo ilikuwa ikisemwa kuwa wameshuka viwango na hawana mvuto tena kwa mashabiki. Kitu kingine nilitaka kuhudhuria ili ninunue kitabu cha Sugu.
Nakumbuka siku ya shoo yenyewe mida ya 12 na dakika kadhaa nilikuwa tayari eneo la tukio sambamba na rafiki zangu ambao pia walikuwa ni classmates wangu. Sio mbaya nikiwataja alafu nitakwambia kwanini nimewataja; alikuwepo Zicco Mwanyaluke, Erick Bamia, Eliud White na Imani Simoni. Nimewataja kwa sababu hawa wote ni wanyakyusa/wasafwa kutoka Mbeya kwa hiyo walikuwa pale kumsapoti mbunge wao (Sugu). Watu wa Mbeya & Arusha ni watu ambayo hupenda kuitanguliza mikoa yao mbele. Ni kitu kizuri kuutanguliza mkoa mbele katika vitu vyenye tija na ambavyo havilengi kuleta matabaka ya u-mkoa.
Pale getini nilikuta toyota hiace ikiuza vitabu vya sugu nikakamata nakala yangu kisha nikakata na tiketi kisha nikazama ndani. Sikukuta watu wengi sana ila kwa kadri muda ulivyokuwa ukizidi kuyoyoma ndivyo watu walizidi kumiminika.
Kwanza kabisa niwapongeze Antivirus kwa kufanya maandalizi mazuri kabla ya shoo na pili waliweza kufanya kile ambacho hakikutarajiwa na wengi wakati wa shoo. Kulikuwa na jukwaa kubwa lenye kiwango na muziki uliokuwa umefungwa ulikuwa ukihitaji kutendewa haki na wasanii waliotakiwa kupafomu.
Ntakuwa sina kumbukumbu sawa sawa kama sitakumbuka mchango mkubwa uliofanywa na kituo cha Times Fm (na DTV pia) kwa kuitangaza shoo hii na kuipa sapoti. Japo nilikuwa miaka michache tangu nilipohamia sikuwa msikilizaji wa Times Fm nafikiri ni wakati huu pia ndipo nilipoanza kuwasikiliza. Namkumbuka mtangazaji Moko Bussiness a.k.a Moko Biashara ambaye pia alikuwa mc wa shoo hiyo. Namkumbuka Hermy B ambaye ni kiongozi wa Times Fm maneno ya kutia hamasa aliyoyazungumza siku hiyo wakati wa shoo kuhusiana na muziki wa Nyumbani.
Niseme kitu, wanahip hop wengi hasa wahafidhina wa Underground Hip Hop wamekuwa wakisema kwamba Hip Hop ya kweli haipo redioni na redio zimekuwa zikizorotesha ustawi wa Hip Hop ya Kweli. Ukweli unabaki kwamba redio ndio njia ya mawasiliano ambayo inaweza kusafirisha taarifa kwa haraka zaidi na kuwafikia watu wengi zaidi kuliko vyombo vingine vya mawasiliano. Kwahiyo wana hip hop wengi kutotumia redio na Tv kutangaza shoo zao ni kupoteza fursa ya kuwatangazia watu wengi zaidi. Inawezekana kuna kupishana itikadi na baadhi ya vituo vya redio kitu muhimu ni kuanzisha vituo vya vyenye mlengo wa kuudumisha utamaduni kama ambavyo redio zenye malengo maalum hufanya.
Vinega waliweza kuona umuhimu wa Redio/Tv kutangaza shoo yao licha ya ukweli kwamba walikuwa na sapoti kubwa ya watu katika mitandao ya kijamii hususani facebook. Nakumbuka pia uwepo wa Mh Mbowe, John Mnyika n.k hata pale muda wa kibali cha kufanya onesho ulipokwisha aliweza kuongea na polisi waongezeke
Yote kwa yote hakuna msanii aliyefanya shoo nzuri kama Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu.
Kwa maoni yangu, sikuwahi kuhudhuria wala kuona kwa hapa Bongo, shoo ambavyo ni “Strictly Hip Hop” watu wamelipia viingilio na bado shoo ikajaza watu kiasi kile. Kwangu mimi mpaka leo Antivirus ndio movement ambayo iliungwa mkono na mashabiki wengi kuliko movement zote ambazo nimepata kuziona Tanzania hii. Huwa najiuliza tu hivi ni nini kiliwafanya wasifikie Malengo yao, maana walikuwa na kila sababu ya kufanikiwa. Katika hili sidhani kama Vinega walikuwa na sababu ya Kumhitaji Dokta Mwaka ili Harakati zao zifike kileleni. Diamond Niache Kidogo tafadhali……

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez

 

 

 

 

 

 
Imeandikwa Na
MALLE HANZI
0715076444
©2016