Vazi la Ali Kiba haliwatoshi King’s Music

Vazi la Ali Kiba haliwatoshi King’s Music.

Waswahili hunena yakuwa “Mwenye moja havai mbili” Semi hii ni yenye uhalisia mkuu katika uisho wa King’s Music. (Hakika)

King’s Music wapo chini ya Ali Kiba na ambapo muundo wake ni wasanii wanne katika upamoja. (Muziki)

Na hatuna shaka katika ujuzi wa uimbaji wao hata kwa udogo, ni wenye ujazo kamili kwa hakika yenye ukuu. (Uimbaji)

Lakini changamoto yao ni ‘Kuvaa vazi la Ali Kiba, ilihali haliwatoshi. Na hatujui ni nani ni mshauri wao na kiongozi mwenye maamuzi juu yao. Au ni Ali Kiba katika upana wa kushauri washauri wenye ujuzi kamili? (Biashara)

Maana mwenendo wao ni ni mwendo wa Kiba wa maringo makuu katika mikakati yake. Ikumbukwe tunaheshimu mno mikakati ya Kiba. (Uhalisia)

Lakini mikakati ya Kiba katika muda mrefu wa utoaji wa wimbo na maisha yake haipaswi iwe ni sehemu ya King’s Music. (Hakika)

King’s Music wanapaswa kutoa kazi nyingi zaidi wapate mzunguko imara katika mtandao na vyombo vya habari. Ikiwa ni sehemu ya kitengeneza mashabiki wao. (Eeh)

Ukimya wao ni wenye fedheha kuu ya kwamba wao ni kama Kiba ilihali hakuna uhalisia. Wao ni wachanga mno, na hawana mashabiki bali wafuasi wa Kiba katika umoja wao. (Uhalisi)

Vivyo wanapaswa wajue yakuwa “Vazi la Kiba haliwatoshi kabisa” Wanapaswa kuamka na kufanya kazi nyingi zaidi. (Naam)

Kujiweka kana kwamba tayari wako usawa na Kiba kisha kuwa chini yao ni sawa na mlevi mwenye kileo katika jitazama ya kioo na kujiona yu sawa. (Fedheha)

King’s Music wanapaswa kuwa na mikakati tofauti na Kiba, wawe na yao katika upana wao. Kuiga au kupangiwa mikakati ya Kiba itawapeleka chini zaidi. (Daima)

#MuzikiNiSisi