Vannesa Mdee na Shilole katikati ya bahari na meli ya mabua.

images

Vannesa Mdee na Shilole katikati ya bahari na meli ya mabua.

Hivi ni kweli muziki umekuwa? Maana kuna vigezo vingi vya kusema muziki umekua, ni wazi ukitazama mwenendo huwezi kusema muziki umekua bali ni msanii mmoja mmoja ndiyo wamekua kimuziki. Yaweza tukawa tofauti katika mchanganuo wa hoja hii, ila hakika muziki kukua tunapasawa kutazama hoja hii kwa mapana sio juu na kuaminishwa na baadhi ya watangazaji wa vipindi vya burudani ambao wengi wametaliwa na mambo mengi ya kinafiki.

Muziki umekuwa kweli? Kama muziki umekua je! inakuaje wasanii zaidi ya wa 3 kushindwa kujaza hata club ya mtaani kwetu Inayoitwa Chinga misamaki? Ni wazi muziki umeshuka na unaendelea kushuka kila leo. Hoja hii naitazama katika mlengo wa muziki kwa ujumla na sio kuhusisha msanii mmoja kama wengi wanavyofanya.

Kuna tofauti kubwa kati ya wasanii wa miaka ya zamani na miaka ya sasa, ambao wengi wao bado ni chipukizi wenye majina makubwa maana ni wazi hawana hata album.

Wengi wamekuwa wakivunja miiko ya muziki wa kizazi kipya kule ambapo umetoka. Sitaacha kusema wasanii waliochangia kukua na kuenea kwa muziki wa kizazi kipya ni wasanii makini na wenye kujali mambo mengi ya msingi kulinganisha na wasanii wa sasa.

Wimbi la mambo ya kipuuzi yanayoendelea sasa katika wasanii wetu wa muziki wa kizazi linachangia kushuka kwa muziki na si kuendelea kama wengi wanavyodhani.

Unafiki ni jambo kubwa linalochangia kushusha muziki huu wa kizazi kipya, ni wazi wasanii wamekuwa wanafiki zaidi kuliko kufanya kazi zaidi ambazo zitawabeba kifua mbele katika mitaa. Wengi wamekuwa wakiamini katika unafiki, najiuliza mara nyingi hivi huu unafiki unawasaidia nini?

Imekuwa kawaida sasa kusikia habari ya kinafiki ambayo yaweza kukustua kabisa lakini baada ya muda unaona ulikuwa ni unafiki. Hali hii imeendelea kukua siku baada ya siku. Na hata kuona wasanii ambao hawafanyi mambo ya kinafiki wanakuwa si wasanii wa kusikika zaidi katika vyombo vya habari. Siachi kujiuliza nani alaumiwe kati ya msanii na chombo cha habari juu ya unafiki?

Wiki kadhaa tumeona unafiki wa Vannesa Mdee na Shilole ambao ulikuwa gumzo katika mitandao ya kijamii hasa katika mtandao wa picha Instagram ambao ni wazi sasa umekuwa ni mtandao uliokosa watu makini mana lugha za matusi ni lugha iliyotawala zaidi.

“Heshima yako unaijenga mwenyewe” lakini hata kuibomoa pia ni wewe mwenyewe, hakika hili lipo wazi katika maisha yetu ya kila siku.

Unafiki wa Shilole na Vannesa Mdee ni wazi ni unafiki ambao umeshangaza walio wengi. Nini kinatokea kwenye muziki wetu mzuri, leo imekuwa wasanii hawawezi kufanya tamasha mpaka wafanye unafiki? Pia kutoa wimbo mpaka wafanye unafiki? Hakika hili si jambo jema kabisa katika kukua na kuendeleza muziki.

Ni wazi mashabiki wamechoshwa na unafiki huu, ni wazi inaonyesha wasanii hawa si wenye kujiamini zaidi bali ni watu wenye uwoga katika nyoyo zao. Wakiamini hawawezi kujaza hata club bila kufanya unafiki, hakika hiki ni kichekesho.

“Muziki wa kizazi kipya umegawanyika makundi mawili kuna wasanii kamili na wasanii batili”hii kwa mujibu wa Prof Jay. Katika wimbo wake wa Tathimini akiwa na Jay Mo.

Ni wazi sikuwa nikitegemea juu ya unafiki huu kati ya Shilole na Vannesa,walichokifanya wasanii hawa ni sawa na kujitekenya na kucheka mwenyewe.  Maana wiki kadhaa tuliona tumbuizo la msanii Lady Jaydee pale mlimani City. Ambalo hakika ni somo katika muziki wa kizazi kipya kwa ujumla. Kwa muitikio mkubwa wa watu hakika imeonyesha ni jinsi gani msanii ukiwa mwenye busara na kuacha unafiki zaidi katika mitandao ya kijamii na hata maisha ya kawaida unaweza ukafanya kitu bora na safi chenye kuweka historia ya vizazi na vizazi.

Ni nani amewaaminisha kuwa unafiki ndio unaweza kujaza katika tumbuizo? Kimsingi mashabiki wemekuwa tofauti ni miaka 2 nyuma. Muziki wa sasa ni wazi unahitaji hekima na kipaji cha hali ya juu, sasa inashangaza kuona wao wakitumia mbinu ambazo hazijengi picha nzuri katika muziki wao.

Ikumbukwe wakati wakitengeza unafiki wao ni wazi lugha za dharau na vitisho zilitawala zaidi. Je unadhani katika unafiki huu wanaweza kujenga kesho iliyobora katika muziki wao?

Ni wazi muziki upo katika bahari iliyochafuka hivyo yakupasa kuwa na chombo sahihi cha kuweza kukuvusha katika machafuko haya. Na kuitengeneza picha yako katika picha ya muonekano mzuri ni vyema kuacha kufanya mambo ya kinafiki, isipokuwa kipaji zaidi.

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez