Uwezo wa Laizer wa Wasafi unatia mashaka.

Uwezo wa Laizer wa Wasafi unatia mashaka.

Wasafi imekuwa na nyumba bora sasa katika muziki wa kizazi kipya, kwa maana ya chati zote za radio na runinga ni lazima kuwepo na wimbo wao kwa namna yoyote ile.

Hili ni jambo jema kibiashara kwa maana ya upana wa kusikika kila leo katika mzunguko mkubwa kwa masikio ya wapenda muziki.

“Kizuri hakikosi kasoro” hakika uhalisia huu unaenda sawa na maisha ya muziki ya mtayarishaji wa muziki kutoka katika lebo ya Wasafi ambaye ni maarufu kama Laizer.

Ni wazi Laizer mwanzo wake umekuwa mzuri mno, ila kadri siku zinavyokwenda ndivyo anapoteza ubora wake kwa maana ya kuwa mtu wa kukopi vyema kazi za wasanii wa Nigeria.

Jambo la kukopi katika muziki sio dhambi, ila dhambi ni kujipa umiliki wa kusema wewe ni chanzo wa kazi hiyo.

Ila  jambo hili la kukopi midundo ya Nigeria haliwezi kutufanya tuwe bora katika muziki wa Afrika kwa maana ya ushindani lakini sisi tunazidi kuwa mabalozi wema wa kutangaza ladha ya Nigeria na sio yetu.

Katika ile kweli kuna kila sababu ya Laizer kufanya anachofanya sasa, kwa maana ya kuwa pekee katika studio za Wasafi. Hivyo mawazo yake yamefika mwisho ila ilipaswa awe na mtu wa ziada katika kuboresha Zaidi.

Ni wazi wakati unamsikia Majani hakuwa peke yake katika pango la Bongo Record bali watu kama Bizman, Ludigo na baadae Soggy Doggy walikuwepo katika kuchangia mawazo na mchango katika kila kazi.

Hapa tumekuwekea wimbo wa Chege Feat Ray ambao chanzo cha mdundo wake ni kutoka Nigeria kwa wasanii ambao wanafahamika kama Blacket.

Sikiliza hapa chini.