Uwekezaji wa biashara nje ya muziki kwa wasanii iwe kitu rasmi.

Uwekezaji wa biashara nje ya muziki kwa wasanii iwe kitu rasmi.

Muziki pekee hautoshi, ila muziki unaweza kubaki kama chanzo kikuu cha msanii kufungua uwekezaji wa biashara nyingine tofauti.

Na hii itaongeza kipato chake lakini hata kutoa nafasi ya ajira kwa watu wengine.

Lakini katika uhalisi uwekezaji katika maeneo mengine nje ya muziki utamfanya msanii kuwa huru katika kuondoa ukata hata pale muziki ukiwa na mkwamo.

Tumeshuhudia wasanii wengi mno wakiwa katika hali mbaya ya kimaisha mara tu pale muziki uwatupapo nje au hata mdau akimzima msanii.

Msanii hupata msoto maana hakuwa amejiwekeza nje ya muziki, na hii ni kutokana na msanii kuona yakuwa kuwekeza nje ya muziki si jambo rasmi.

Lakini kama msanii atajivika ufahamu wa kuwekeza nje ya muziki ni jambo rasmi hakika ataishi katika uzuri kwenye nyakati zote za muziki hata nje ya muziki.

Hivyo “Uwekezaji wa biashara nje ya muziki kwa wasanii iwe kitu rasmi”

Na pongezi zetu kwa wasanii wote ambao wamewekeza nje ya muziki. Twasema Pongezi kubwa.

#TuzungumzeMuziki