UTATA BAINA YA NASH EMCEE NA FID Q

nash

UTATA BAINA YA NASH EMCEE NA FID Q

Miaka kadhaa iliyopita FID Q alikua akiwaalika wasanii wanaorap hasa wale               ma emcee kutoka katika utamaduni wa hiphop katika kipindi cha fidstyle Friday ambapo ma emcee  walionyesha uwezo wao, walitoa elimu pamoja na kujadili changamoto mbalimbali kata kiwanda cha muziki.Binafsi nilishtuka kidogo baada ya kutomuona Nash mc kwenye kipindi kile,unaweza ukauliza kwa nini hukushtuka kutokuwepo kwa Chindo Man,lakini ukweli ni kwamba Chindo alikua ughaibuni kwa muda ule kwa mujibu wa Maelezo ya mtengwa mwenzie JCB alipofanya mahojiano na Fid q katika fidstyle friday.Lakini pia kuna tetesi kwamba kuna sintofahamu inaendelea kati ya Chindo man na Fid q baada ya Chindo kukomenti kwamba  Fid q ni wack katika post moja hivi Facebook kipindi kile cha matokeo ya uchaguzi mkuu.OK tuachane na Chindo turud kwa Nash mc.

Movie ilianza rasmi pale Fid q alipoulizwa na shabiki mtandaoni kuhusu sanaa ya Nash mc ambapo shabiki aliuliza “Unaamini Nash mc ana sifa kamilifu za kuitwa mc?” Fid q akajibu ” Honestly… Sijawahi kumsikiliza so sina jibu la swali lako”.Kauli hii iliwashtusha wengi na ikapelekea baadhi ya watu kuhisi kwamba hakuna mawasiliano mazuri kati ya Nash mc na Fid q.

Inaonekana wazi kabisa Nash hakupendezwa na kauli     ya  Fid q na katika mixtape yake ya “CHIZI” Nash ameiongelea hii issue kama Mara mbili hivi.Kwenye wimbo wake wa asiyehusika na hiphop kuna sehemu amesikika akisema “Uwezo wenu inaonekana bila  media mnapwaya/wanaosema hawanijui ni wazi wananigwaya”. Pia katika wimbo wake wa mwisho             ” maswali ya kiwaki” katika orodha ya nyimbo zake kwenye mixtape ya CHIZI kuna mstari amesikika akisema        ” ambao hawanijui ni wa kuja na  hawanisumbui”.Ikumbukwe pia Fid q aliwahi kunukuliwa akisema ameinspire asilimia 98 (98%) ya wasanii wa hiphop bongo,takwimu ambazo Binafsi sidhani kama zina ukweli ndani yake na sijui Fid q hizi takwimu alizitoa wapi.

Nash pia aliendeleza mashambulizi ambapo mwanzon mwa mwaka 2014 aliandika “tweets” ambazo zilishtusha watu wengi akiwemo mtangazaji  Jabir Saleh kipindi yupo Times FM katika kipindi cha the Jump off alinukuliwa akisema ” Leo Nash mc ameandika tweets za moto, ameandika mambo flan ya kushtusha hiv …. “. Nash aliandika tweets nyingi sana  nyingine inasemakana zilikuwa zikimlenga rapper wakazi.Tweet mojawapo ni Hii ” Nimeanza sanaa muzik kurecord kwa Hendrico sound crafters elfu 37,fala wako unaemuaminia hajagusa Dar!” Wana utamaduni wa hiphop wanadai hiyo kauli ilikua ikimlenga Fid q pamoja na wakazi,hapa Nash anamwambia wakazi kwamba huyo emcee Fid q unaemuaminia ni fala tu! ambapo   tunaona Nash akijitamba kuwa yeye ni “born town” akimaanisha yeye ni mtoto wa mjini toka kitambo.Na Hii yote ilikuja Baada ya wakazi kupost picha alizopiga na KRS ONE pamoja na RAKIM ughaibuni Marekani ambapo Nash mc                   aka comment kwa kusema kupiga picha na hao Hiphop giants / legends(KRS ONE & RAKIM) haimaniishi kuwa wewe ni emcee kwa sabab hata shilole anaweza akapiga nao  picha ingawa sio emcee .Tweets zilikua nyingi unaweza kuzitafuta katika mtandao,lakini mwisho wa siku Nash mc alikanusha kwamba hizo tweets haziashirii ugomvi wowote na kwamba yeye hana ugomvi na msanii yeyote Tanzania.

Nash pia amewahi kuandika katika   Twitter ” msanii wa hiphop unalewa mpaka  unashindwa kufanya show,unazomewa kwenu?????? Pumbavu!”.       Na Hii ilikua ikimlenga Fid q kipindi kile alipopanda stejini akiwa amelewa jijini Mwanza lakin baadae Fid q katika mahojiano kwenye kipindi cha Mkasi pale EATV alieleza kwamba hakulewa kwa  makusudi bali kuna mtu alimwekea kilevi bila yeye kujua alipokua back stage.

Pia juzi juzi tu katika wimbo wake wa hasi 15 Nash alisikika akisema ” lipstick,shedo ndo mnakua hivi rasta?/ ww ulikua wapi nilivyokua hapa?/Pale  jite ute kila wiki matamasha……..Hapo   tunaona Nash akimdiss Fid q kuwa alijipaka lipstick kwenye video yake ya Bongo Hiphop,Lakini Fid alipoulizwa kuhusu hili alijibu hivi namnukuu ” Sijapaka lipstick zile ni lips zangu baada ya kupigwa na effects kwenye editing”
Lakini tunamuona tena Nash katika mstari huo hapo juu anajitamba kwa Mara ya tatu kuwa yeye ni” born town ” kitambo na kwamba  ameanza muzik kabla Fid q hajafika Dar!!!!.

Ya mwisho ni Hii Nash aliposema” Heshima kwa zavara /,lindu na Hashim mmeuachaje utawala/ mpaka icon ya Hiphop ya bongo wanapewa mafala/ mnawapa sana vyeo hawa watu mwa wa media…..Nimeona watu wengi wakidai kwamba Hii nayo ilikua imemlenga Fid q,lakin binafsi naona hapa Nash hakua specific sana na inaonekana ni kauli ambayo imelenga  zaid ya mtu mmoja kwa sabab watumwa wa media ni wengi,labda Nash siku moja atatupatia ufafanuzi zaid kuhusu huu mstari.

Ukiwafuatilia  wote wawili utaona wana safari ndefu kidogo,ebu tuanze na Nash

Nash alianza Sanaa akiwa na umri mdogo sana nyimbo yake ya kwanza kwa Maelezo yake ni kwamba alirecord akiwa bado yupo shule ambapo alimshirikisha dullysykes na ngoma ilikua inaitwa kisa cha mwanafunzi kama sijakosea.Baadae  alitoa nyimbo nyingne na akafanya show kadhaa mjini Dar es salaam na kuna wimbo ambao aliufanya yeye na kundi lake  uliwekwa kwenye  mkanda wa VHS ambao ulikua ukiandaliwa na wahindi kipindi kile kama mnakumbuka.Baada ya hapo Nash alikua  kimya sana mpaka mwaka 2009 ambapo Nash alirudi kwa speed ya ajabu sana na akafanikiwa kutoa mixtape 2,album 1,na EP 1.Pia tumeona amekua akifanya mihadhara katika vyuo vikuu ambapo amekua akitoa elimu kuhusu hiphop na ni emcee aliyekataa  katu katu utumwa na unyonyaji katika Sanaa yake,tumeona amekua akijitengenezea mifumo yake  mwenyewe ya kutengeneza pesa kupitia hiphop na pia tumeona ni emcee ambae amekua akiutetea sana utamaduni wa hiphop na amekua akipinga sana upotoshwaji unaofanywa kuhusu huu utamaduni.

Tukija kwa Fid q mpaka sasa amefanikiwa kutoa album 2 tu ile ya  Vina Mwanzo  Kati na mwisho pamoja  na Propaganda.Fid q amekua akifanya vizur pia nae tumeona alikua  akitoa elimu kupitia ujamaa hiphop darasa, lakini hivi karibun jamii ya watu wa hiphop kwa kiasi flan hivi wamepoteza imani na Fid q. Sanaa ya Fid q imekumbwa na dhoruba hivi karibun na Hii ilikua Baada ya kutoa video yake ya bongo hiphop ambapo watu wengi wanadai video hiyo  haijakaa ki hiphop na kwamba haijaakisi kile kilichopo kwenye audio yaan kwamba kulikua hamna uhusiano kabisa kati ya video na audio, ambapo kwenye Hii video ukiangalia utawaona big booty hoes  wakiwa nusu uchi na nimeona watu wengi wamediss sana hiki kitu.Pia  inasemekana Fid q alijipaka lipstick kwenye hiyo video,lakini Fid q mwenyew alikanusha kwa kusema kwamba zile ni lips zake mwenyew na kwamba hakupaka lipstick Bali ilikua ni effects tu kwenye editing.

Pia nimeona watu wamekua wakiudiss wimbo wa ” walk it off” wakidai kwamba sio wa mahadhi ya hiphop na hata video yake sio ya ki hiphop

Binafsi Mimi sipo upande wowote sipo kwa Fid q wala kwa Nash naomba nieleweke vizur hapo.Pia watu kupishana kauli na kutofautiana ni kitu cha kawaida katika maisha ya kila siku lakini mwisho wa siku suluhisho ndo kitu cha muhimu zaidi,hivyo nategemea siku moja Nash na Fid wawe kitu kimoja na waunganishe nguvu katika kuusogeza na kuupeleka huu utamaduni mbali zaid kama ilivyokua kwa KRS ONE na Marley Marl waliokua na bifu Kali kwa muda wa miaka 20  lakini mwaka 2007 walipatana na wakashirikiana kwa pamoja kutengeneza album ya ” Hiphop lives” moja kati ya album bora kabisa kuwahi kutokea kwenye ulimwengu wa hiphop.

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez

Imeandikwa na

O.G Golden Age Technique