Usichukizwe na ukweli, maana fimbo ya maonyo hutia hekima. (Billnass)

Usichukizwe na ukweli, maana fimbo ya maonyo hutia hekima. (Billnass)

Nyakati zote mswahili husisitiza kwa sauti ya juu yakuwa “Mtu mzima akivuliwa nguo hadharani huchutama”

Yakupasa kufikiri mno ili uweze pata maana halisi yenye uhalisia juu ya semi hiyo ya mswahili.

Mfadhaiko wa Billnass ni mkubwa mno, kiasi cha kushindwa kupokea simu ilihali kuandika ujumbe katika mtandao wa picha ‘instagram’ na kufuta ndani ya muda mchache. (Mfadhaiko)

Usifedheheshwe na makosa bali kujifunza kuto kurudia kosa nyakati nyingine.

Lakini katika kweli yenye kweli yampasa Billnass aidharau aibu ili aweze kuishi katika uhalisia wake.

Kuandika posti na kufuta haimsaidii , ila kuweka hadharani radhi yake na hakika waswahili ni waungwana hivyo wataipokea kwa mikono miwili.

Lakini ni vyema ajue yakuwa “Kila chanzo kina chanzo” ilihali matokeo hufanya tuchukie chanzo”

Chanzo cha kujirekodi video ile ni mapenzi katika penzi wakiwa penzini, lihali mwisho wake umekuwa kisa katika mkasa wa fedheha. (Soni)

Lakini je! yupo mswahili ambaye haamini katika radhi ya hadharani? hakika hakuna.

Na kilichotokea kwa Billnas ni fimbo ya onyo juu ya sanaa yake katika kesho yake na vizazi vyake kwa mlengo wa kumpa hekima ya kuwaza kwa upana maisha yake ya faragha.

Maana nyakati zote “Mambo ya nyumba, ni kinga” Ilihali “Mchezea na tope humrukia” Tafakari.

TuzungumzeMuziki.