Ushindi wa Joh Makini ni kujua bidhaa ipi iwe sokoni kwa nyakati kamili.

Ushindi wa Joh Makini ni kujua bidhaa ipi iwe sokoni kwa nyakati kamili.

Ipo tofauti ya midondoko na tungo tangu enzi za ‘Hao’ mpaka sasa ‘Simwachii Mungu’ kwa upana wa Joh Makini.

Mara zote hunena yakuwa kipaji na ujuzi wa muziki ni kitu mosi, lakini kuuza bidhaa ya muziki kwa wateja ni kitu pili.

Inahitaji umakini mno kujua uhalisi huu na katika kweli yenye kweli wasanii wengi ni wenye anguko kubwa la kushindwa kuweka bidhaa zao kulingana na nyakati kamili.

Hivyo hubaki na ujuzi wao katika vifua vyao. Lakini kwa Joh imekuwa tofauti kwa maana kila leo amekuwa yukatika soko tangu alipofahamika kwenye uwanja wa muziki.

Katika uwazi ushindi wa kuwa kwenye soko nyakati zote ni namna ya kujua namna ya soko liendavyo kwa maana bidhaa ipi iende sokoni kwa nyakati ipi.

Ingekuwa ni anguko kwake ambapo angetaka soko la sasa liende na usawia wa wimbo kama Hao au ufalme kama sio Dakika 90 pia.

Soko haliko huko soko lipo ambapo yeye yupo katika ‘Simwachii Mungu’ kwa maana ya mdundo wenye ujazo wa kusikiliza na kucheza katika nyakati mosi.

Michano yenye ladha na miyepesi yenye kushikika kwa uwepesi ndipo soko lilipo, na ikumbukwe muziki ni sanaa pana hivyo msanii hupaswi kuwa katika boksi.

Bali kufanya nje ya boksi kwa upana wa ujuzi wako wa sanaa na usimame imara katika upya wa kuendana na soko.

Haipaswi msanii ajifunge katika kifungi kimoja bali kufanya katika uwezo wake awezao. Ni wazi ‘Simwachii Mungu’ ni wimbo mzuri kuanzia Audio pamoja na Video.

#TuzungumzeMuziki