Upekee wa Shaa unafanya akumbukwe kwenye muziki, lakini Shaa yuwapi?

Upekee wa Shaa unafanya akumbukwe kwenye muziki, lakini Shaa yuwapi?

Hakika upekee wa Shaa ndiyo ambao unafanya wajuzi wa muziki wamkumbuke vyema katika nyakati hizi.

Maana kama angelikuwa hana upekee hakika si rahisi kumkumbukwa kwa maana ya kuwepo mbadala wake.

Na katika zama hizi ni wasanii wachache mno wenye upekee katika uimbaji na hata maisha yao nje ya uimbaji. Hakika Shaa ni mmoja wao, wengi ni katika mfanano.

Ukimya wake ni wa muda mrefu na tukikumbuka kumbukumbu mara yake ya mwisho kutoa wimbo ni 2016 na wimbo ulikuwa waitwa ‘Sawa’.

Baada ya hapo ukimya umekuwa mrefu si wa utoaji wa nyimbo tu bali hata matumizi ya mtandao ni katika hali ya udogo mno.

Ni wazi wajuzi wanaamini katika kipawa chake na aina yake ya muziki na matamanio ni makubwa ya kutaka arejee tena. Maana alishafika pazuri katika soko,hivyo ukimya wake unafanya arudi nyuma zaidi.

Muziki wetu haupo sawia kwa msanii kama atakuwa anakaa kimya zaidi ya miaka 2, hivyo ni vyema Shaa amke na aweze kufanya muziki katika kweli yenye kweli nafasi yake ikubwa katika muziki huu.

Muziki unamuhitaji Shaa kwa hali ya ukubwa, hivyo ni vyema Shaa afanye jambo katika nyakati hizi kulingana na uwanja ulivyo.

#TuzungumzeMuziki