‘Umri si namba tu bali maarifa na hekima’ Tid

‘Umri si namba tu bali maarifa na hekima’ Tid 

Waswahili hunena yakuwa “Bure ni malipo pasipo na sikio” Semi hizi hutupa uhalisia wa mengi katika nyakati zote. (Maisha)

Tumesikitishwa na picha kadhalika picha nyongefu ya msanii Tid katika ugomvi wake ambao umepeleka kuumizwa zaidi. (Sikitiko)

Jambo hili si jema kabisa, na kama Tid angekuwa na busara hakika leo hii wala asingekuwa fedheha katika maumivu makuu. (Soni)

“Jema lipo baya lajia nini?” angelikuwa na hekima basi wala isingekuwa fedheha lakini maarifa ya kuepuka ugomvi yangemtawala hakika ingekuwa ni amani kuu. (Busara)

Tazama ugomvi umemuathiri kiasi gani, kwa maana leo alipaswa awepo Ladhani Efm lakini haikuwa maana amepata majeraha. (Ujinga)

Umri wake ukilinganisha na wasanii ambao walianza pamoja wengi wao kama Mwana Fa, Ay, Gk na wengine wengi wapo bize katika biashara zao nyingine kubwa. (Kabisa)

Tid bado yuko na utoto na kileo cha umaarufu ambacho hakina maana wala faida katika endelezo lake kuu. (Anguko)

Ni kampuni gani iwekeze kwake? Tid ni chapa iliyochafuka mno kwa namna ya mengi yake katika lugha kali na fedheha. (Huzuni)

Ni wazi “Hakuna zaidi mbovu” lakini Tid ni zaidi yenye ubovu mkuu yapasa kujitafakari mno bila umakini atabaki kuwa katika kundi la maarufu wasio na maana wala maana. (Muda)

Yote ya yote pole zetu ziwe juu yake katika mapito haya yenye maumivu, tunaamini kwa upana huu amejifunza jambo. (Kweli)

Na twajua kabisa yakuwa “Hasara humfika mwenye mabezo” la! hasha umri si namba bali maarifa na hekima. (Uisho)

Lakini Q Chief kuweka posti yenye kufurahia changamoto za Tid jambo baya zaidi, kwa umri na nafasi ya Q Chief hapaswi kushangilia bali huzuniko. (Kabisa)

Lakini shangilio lake litampa mahojiano mengi twajua, ila ni mahojiano ambayo hayatakuwa na maana wala maana yenyewe kwake. (Iko wazi)

Kheri ya mrama, kuliko kuzama ni wazi Q Chief anajizidi kujizamisha katika kundi kuu la wajuzi wenye muziki wasiopagawa na matendo. (Naam)

#MuzikiNiSisi 

Zaidi www.tizneez.com kiunga juu.