Umewahi kutafakari juu ya Roma Mkatoliki na One The Incredible katika wimbo mmoja?.

Umewahi kutafakari juu ya Roma Mkatoliki na One The Incredible katika wimbo mmoja?.

Wajuzi huiona tofauti kubwa katika wasanii hawa wawili ingawaje wote wapo chini ya mwamvuli wa hiphop.

Tofauti ni katika aina ya uandishi lakini hata namna ya aina ya michano kwa maana ya midondoko juu ya kila wimbo.

Roma amekuwa ni mzito katika ubadili wa midondoko lakini One ni mwepesi katika ubadiliko wa midondoko.

Ila hata katika uandishi Roma ni mwenye kuandika mistari yenye uwazi zaidi ilihali One ni mwenye mistari mingi yenye kuhitaji tafakuri kuu.

Je! wasanii hawa wakiwa katika wimbo mmoja itakuwaje?

Wajuzi wanaamini mpishano huo hautaleta matata bali kupata wimbo mzuri, ila kuwe na uchaguzi wa mada halisi.

Na tayari One ameshaonesha nia ya kutamani kufanya kazi na Roma, hivyo lolote linaweza kutokea nyakati zozote.

Ni wazi wajuzi ni wenye kutamani mno siku katika kusikia wimbo ambao utawakutanisha wakali hawa.

Je! wewe unatamani kuwepo kwa wimbo wa pamoja kati ya One na Roma?

#TuzungumzeMuziki