Umaarufu unaambatana na upumbavu?

images

Umaarufu unaambatana na upumbavu?

Muziki wa kizazi naona umegawanyika katika makundi mawili.Kuna wasanii wanaojiheshimu pia wale wasiojiheshimu, msanii mwenye akili utafakari kabla hajafanya jambo na msanii msanii asiye na akili hufanya jambo bila kutafakari.

Yamkini unaweza ona nimetumia lugha kali, lakini sio lugha kali kama unaelewa maana ya neno upumbavu. Ila ni vyema kujiuliza umaarufu unaambatana na upumbavu?.

Neno upumbavu lina maana nyingi katika uhalisia, na maana zake zote ni upumbavu. Neno mpumbavu lina maana ya mtu wa hovyo hovyo zaidi, asiyekuwa na utashi (Akili) ya kutosha ambaye ndani yake ana uwendawazimu ndio unaofanya kazi au kummiliki mhusika mpaka matunda au matokeo ya neno mpumbavu kuanza kufanywa  na mwanadamu ili watu kuyaona  na hata kumpa jina hilo.

Pia hata katika maandiko matakatifu Mathayo 7 : 24 -27 imeeleza vyema kuhusu aina ya mtu mpumbavu.

Kazi kubwa ya uandishi kuandika mengi yenye kujenga jamii zaidi, ila wapo wachache wenye mioyo ya kusifia takataka mpaka ukaona ni nzuri na zinafaa kwa matumizi mengine, hivyo ukaendelea kukaa nazo ndani kama sio kutupa.

Hii nitaisema kila iitwapo leo, jamani tusiuone ukweli kama ni ubaya kwenye maisha yetu. Heshima yako ya maisha yajayo unaitengeneza leo hii. Ni ngumu sana kufanya mambo mabaya leo na ukataka watu waje wakuheshimu katika nyakati zijazo.

Msanii ni kioo cha jamii, kauli hii imetumika katika mifano iliyomingi kwenye sanaa ya muziki wetu wa kizazi kipya. Hakika nasema kwa nguvu zote wasanii ambao ni kioo cha jamii ni wachache mno, ila wengi wao ni vioo vilivyopasuka mbele ya jamii.

Usanii ni wito pia, wapo wengi ambao huiharibu wenyewe heshima mbele ya jamii tena kwa nguvu zao, lakini cha ajabu hutaka baadae wapate heshima ya hali ya juu. Mara zote watu hukuheshimu na kukuchukulia vile ambavyo unajiweka mbele yao.

Wapo wengi katika mitadao ya kijamii ambao husema “Wengi wanatumia kivuli cha muziki kufanya mambo mabaya zaidi” kauli huwa siiungi mkono hata kidogo maana mara zote inakuwa imelenga zaidi upande wa kike. Ila katika uhalisia maneno haya huanza kwa vile vitendo vya baadhi ya wasanii wa kike kuweka picha za uchi kama sio nusu uchi katika kurasa zao za mitandao ya kijamii, hivyo hufanya baadhi ya watumiaji wa mitandao hiyo kutoa lugha kali na kupitisha hoja yao ya wasanii hawa kufanya matendo mabaya sio muziki.

Tangu kuwepo kwa mitandao ya kijamii imekuwa kawaida kuona vioja vyenye kila aina na viashiria vya upumbavu juu ya baadhi ya watu maarufu. Tumebahatika kuwa na watu wengi maarufu, ambao katika uhalisia hawajui jinsi ya kutumia mitandao ya kijamii.

Ikumbukwe muziki huu wapo wakongwe waliofanya baadhi ya wazazi wakawapa ruhusu watoto wao waimbe. Lakini kile kinachofanywa sasa na hawa baadhi ya watu maarufu kitafanya wazazi wengine waruhusu watoto wao waimbe?.

Matendo yanayoendelea sasa imefanya nijiulize kuwa umaarufu unaambatana na upumbavu?. Ni jambo la kawaida siku hizi mtu maarufu kuweka picha zake za faragha katika kurasa za mitandao ya kijamii. Pia ni kawaida kabisa kuona mtu maarufu kaweka picha inayoonyesha nguo yake ya ndani au maungo yake kabisa.

Ni mwaka sasa umepita tangu kuona zile picha za msanii wa muziki wa kizazi kipya Shilole, ambapo picha hizo zilionyesha maungo yake ya sehemu za siri yakiwa nje. Tumbuizo hilo lilifanyika huko nchini Ubilgiji

Baraza La Sanaa Tanzania lilipaza sauti yake na hata kuamua kumfungia mwaka mzima. Lakini cha ajabu haikuwa kama vile maagizo yalivyotoka maana Shilole alionekana katika majukwaa ya siasa siku chache baadae. Hata hivyo ni wazi kituo kimoja cha radio kilitumia nguvu kubwa kumuombea msamaha na hata kumpa muda mzuri wa kueleza vile ambavyo tukio lilitokea. Pia hata baadhi ya wasanii akiwemo Snura hakusita kupaza sauti yake kumuombea msamaha msanii mwenzake Shilole.

Wengi tulitarajia kuona mabadiliko makubwa kutoka kwa watu hawa maarufu, lakini haikuwa vile ilivyokuwa katika matarajio ya walio wengi. Binafsi nimeona hali inazidi kuwa mbaya zaidi mana hata wale watu maarufu ambayo sikuwahi kuwafikiria niliona wakiweka picha zisizofaa katika mitandao ya kijamii.Inanipa tabu kufikiri nini hasa huwa wanataka au faida gani wanapata kuweka picha zao zisizofaa kwenye mitandao ya kijamii?

Hakika idadi imeendelea kukua, imefika hatua hata kutazama ukurasa za baadhi ya watu maarufu inabidi utazame ukiwa umejifisha, maana ni kawaida kukuta mambo yasiyofaa. Umesahau kuhusu chura ya ambavyo alikuwa anafanya msanii Snura?Je unaweza kutazama hadharani? Video ya Shilole akiwa Tanga pamoja na picha yake iliyonyesha eneo kubwa la mwili wake sehem ya nyuma? Huku mwenyewe akionekana mweye tabasamu yamkini amefanya jambo jema zaidi.

Kuna maswali mengi najiuliza binafsi, hivi kuweka picha za nusu uchi au video za ajabu je ndio kwenda kimataifa?. Siamini katika upumbavu zaidi ila naamini katika kazi bora ambayo ni wazi itafanya uende katika ngazi za kimtaifa ukiwa na heshima yako.

Ni vyema pia ukumbukwe wewe ni mama au baba wa baadae, je unajua matendo unayofanya yatakuja kumnyima mwanao uhuru wa vitu vingi?.

Tunaweza kuwa tofauti kimtazamo, ila ni vingumu kuwa tofauti katika kusema ile iliyo kweli ambayo itachingia kweli na kuleta mambo yenye tija katika jamii zetu na hata kukuza sanaa katika nidhamu ya hali ya kweli.

Tazama hapa Post tata za msanii Shilole

#SayMaName @ummykitwana

A video posted by Shishi bybee /she roll it (@shilolekiuno_badgirlshishi) on


Malkia wa igunga mie nipo tayari kwa show pale harbours club thanks @jokatemwegelo kwa nywele pia my lv dogo @marwakibaso kwa make up

A photo posted by Shishi bybee /she roll it (@shilolekiuno_badgirlshishi) on

 

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez