Ulazima ulikuwa upi wa Fid Q kumrekodi video mama yake na GodZillah? (Ulizo)

Ulazima ulikuwa upi wa Fid Q kumrekodi video mama yake na GodZillah? (Ulizo)

Mosi furaha yetu ni mama yake na Zilla kupatiwa msaada mzuri katika endelezo la maisha katika kile atakachokifanya. (Naam)

Lakini chukizo letu kuu ni video ambayo mama akionyeshwa vyema kabisa katika mapokeo ya fedha hiyo. (Kwanini)

Busara ni kumkabidhi bila kumrekodi, hivi unamrekodi kwa maana ipi? Kabisa katika hali ile ya mama unapata ujasiri wa kumrekodi na kuweka mtandaoni? (Soni)

Ni windo la ‘Likes’ na ‘Comment’ hakika ni jambo lenye jazo kamili la puuzi nzito. (Fedheha)

Picha tosha ni ile ya Fid Q na Mkuu wa Mkoa ingetosha kwa upana wake kabisa, lakini video ambayo inamuonyesha mama akiwa hana chembe ya tabasamu si njema. (Hakika)

Lakini mitandao isifanye kupoteza utu na busara katika kila kitu kuweka mtandaoni, funzo ni katika chaguzi sahihi. (Uhalisia)

Kwa namna tunaheshimu ufahamu wa Fid Q imetupa mafikirio mengi ni kwanini ameona ni sawia kabisa kuweka video ile. (Shangazo)

Ni hofu ya watu kunena kuwa hazijafika? Kwani unapaswa kufanya jambo kufurahisha watu ama kufanya jambo kwa usahihi? (Jamani)

Au umefanya hivyo kwa ajili ya Mkuu wa Mkoa kuwa hajakuwepo? Vivyo ulirekodi ili uweze kumuonyesha umefika? Ulizo)

Lakini kama Mkuu wa Mkoa alikuwa hakuamini kuwa mjumbe wake basi angekwenda mwenyewe ama mtu mwingine. (Ndiyo)

Fid Q unataka kutuaminisha yakuwa Mkuu alihitaji kipande cha picha ya video ya makabidhiano ili kujiridhisha? (Hapana)

Lakini fid Q ni nani mpaka kutumiwa? (Ulizo). Mkuu wa mkoa haoni kama ingekuwa busara endapo angehusisha chama cha wasanii wa kizazi kipya (Tuma) kupeleka pole yake kama yeye anamajukumu mengine? (Au)

Na tunanena kuhusu Chama kwa maana “Umoja wa wasanii ndiyo njia” na umoja unajengwa na wasanii ndani ya chama. (Hakika)

Yote ya yote ni vyema tujue utu katika vitu tufanyavyo, jambo baya ni utumizi wa tatizo katika ongezo la umaarufu wenye pole na huruma lakini ubaya ni katika fedheha ya mtu. (Mbaya)

Lakini ndugu zetu mwapaswa mjue yakuwa “Msigombane na mkwezi nazi imeliwa na mwezi” (Tutaona Mengi)

#MuzikiNiSisi