Uko wapi umoja wa wasanii wa hiphop? (Ulizo)

Uko wapi umoja wa wasanii wa hiphop?  (Ulizo)

Wenyewe wanahiphop wanalo group lao la WhatsApp ambao wamejiweka huko kwa upana wao. (Ndiyo)

Hiphop Community ndiyo jina kamili la Group lenyewe. Mwanzo wao ni katika kusanyo tu ambalo chanzo chake ni matumaini. (Eeh)

Lakini matumaini yakapotea na sasa limebaki zaidi katika michango ya rambirambi si katika kuinua hiphop kwa ukubwa wake. (Kabisa)

Kuinua kwa ukubwa wake wake ni namna ya kushikana mikono wao kwa wao katika kazi zao. Na hapa ni kwa maana ya msanii wa hiphop ataopo album au kanda mseto na wenzake kuipa nguvu (Matangazo)

Ni ngumu kufanya hivyo kwa kuwa tunajua ni biashara moja wafanyayo, yani ni sawa Tigo azungumze kuhusu Vodacom. Lakini kwa kuinua zaidi hiphop ingefaa na wala isingeleta matata ukizingatia wapo group moja. (Hakika)

Lakini tokeo lake ni ukimya mkubwa ambao hauna maana wala maana yenyewe. Lakini uhalisi ni kwamba kama album na kanda mseto zikifanya vyema sokoni ni wazi biashara ya hiphop inakuwa kubwa zaidi. (Naam)

Lakini leo Wasanii ambao wameposti kuhusu bidhaa za hiphop kwa maana ya album na kanda mseto ni katika uchache wenye soni kubwa. (Fedheha)

Wengi wako na ukimya kana kwamba hakuna ambacho kinaendelea kwenye muziki wa hiphop. (Ajabu)

Na tunaona ambavyo msanii kama Mr Blue akiendelea kutangaza kazi ya Maalim Nash Mc kwenye mitandao. Hakika hili ni jambo jema mno. (Kabisa)

Na wasanii wa hiphop kazi yao kubwa ni kusema huyu si hiphop kabisa, huyu ni waki hana lolote. (Uhalisia)

Lakini wao wasanii wa hiphop na wenye kutumainiwa kuwa ni bora kwenye hiphop wanatoa nguvu ya hiphop kwa wasanii wenye bidhaa mkononi? (Aah Wapi)

Wapo kimya mithili ya chemchem iliyokauka. Lakini unafikia wa kunena kando yakuwa aah album mbovu ile, kanda mseto ile ya kawaida sana, aah mtu mwenyewe anauza kwa WhatsApp tu. (Kunafikia)

Kama wewe ni msanii wa hiphop na unamapenzi na hiphop si unatoa njia ya kuuza katika kujenga, kwanini uwe mnafikia hodari pembeni? (Shangazo)

Lakini twaambieni uhalisi sisi Tizneez tumekuwa na ukaribu wa wasanii karibu wote wote wa Hiphop ,ni wazi ni wanafikia kuliko ujuavyo. (Kweli)

Sijui kunafikia kunatoka wapi? maana ni wazuri mno katika elezo la nje lakini uisho wa ndani ni wenye fedheha kuu ya kunafikia. (Soni)

Lakini wala hatuna shangazo kuu kwa maana twajua yakuwa “Uzuri wa godoro nje, undani mpana pamba” (Ufahamu)

Leo wasanii ambao mnajua ni wakubwa wa hiphop mmeona wapi wakizungumza na kusifu uwepo wa bidhaa za hiphop? (Hakuna)

Wengi wao vinywa vyao ni vyepesi nyakati hizi ni katika kusifu mialiko ya chakula na vikao vya usengenyaji kuliko bidhaa walizonazo kwenye uwanja wa hiphop. (Ajabu)

Ni wazi kama kweli wasanii wa hiphop mnataka hiphop irudi na iwe katika kila usikivu wa mtu basi lazima mvue koti kubwa la kunafikia. (Ndiyo)

Na vazi la uhalisi na ukweli wa hiphop liwatoshe basi hapo endelezo jema ni katika upana wa faida kamili. (Biashara)

Kama mna group na hakuna hata cha maana cha kujadili, kuendeleza na kupeana nguvu katika bidhaa ni wazi hapo ni kunafikia tu hakuna cha ziada. (Eeh)

Kama nyinyi wenyewe tu hamna nguvu ya kuzungumza bidhaa zenu tarajio ni nani azungumze? Tunawakumbusha tu “Huwezi kwenda kwa jirani pasina kutokea kwako” (Daima)

La! Hasha tunajua yakuwa “Ukiongea chenye busara wasio na busara watapinga” (Uhalisia)

#MuzikiNiSisi