Ukimya wa Ali Kiba ni katika mipango mikakati yake

Ukimya wa Ali Kiba ni katika mipango mikakati yake.

Mkakati/mikakati katika upana wa maana wa yakuwa ni mpango maalum unaoandaliwa kwa ustadi mkubwa ili utumike kama njia ya kufikia lengo fulani. (Naam)

Mashabiki katika uwingi ni lawama juu ya ukimya wa Ali Kiba hasa katika utoaji wa kazi zake katika uchache wa nyakati ndefu. (Huzuni)

Lakini tunapenda mjue yakuwa kila mtu ni katika mikakati yake juu ya kile afanyacho, vivyo kutaka atoe wimbo kwenye nyakati fupi hapo tutakuwa ni wenye kumpangia mikakati. (Kabisa)

Ilihali “Kuzungumza ni fedha, la hasha kukaa kimya ni dhahabu” Lakini kukaa kimya kwa muda mrefu kunatoa upana wa kutengeneza kazi yenye ujazo wa uisho wa nyakati zote. (Ubora)

Na pia mashabiki wanapaswa kujua yakuwa msanii anaweza kukaa kimya na thamani yake ikapanda na hii ni kulingana ni mikakati katika uongozi. (Ufahamu)

Na hata ufanyaji wa shoo waweza kuwa ni katika uchache lakini wenye ujazo wa faida kuu sio shoo nyingi katika mchundo. (Okoteza)

Kimya kibaya ni kile ambacho hata kazi zako zilizopita zinakuwa hazipo katika mzunguko. Au hata wale wenye kutoa kazi mpya washindwe kuzungmza juu yako. (Hofu)

Lakini “Mwenye utambuzi mwingi hukaa kimya kwa nyakati” (Daima) 

Vivyo sisi hatuoni kama kuna changamoto katoka upana wa Ali Kiba kutoa kazi katika nyakati ndefu zaidi, maana tunamini hiyo ni katika mpango wake. (Mikakati)

#MuzikiNiSisi