‘Ukidhamiria kumuamsha mtu hakiki kwanza kulala kwake’ Nay wa Mitego.

‘Ukidhamiria kumuamsha mtu hakiki kwanza kulala kwake’ Nay wa Mitego.

Ni wazi unaweza kupoteza muda na nguvu katika kushauri mtu asiyejua maana wala ukubwa wa ushauri wako. Ila yapasa usiache katika kutengeneza kesho zenye maana kubwa katika maisha  ya Sanaa na nje ya Sanaa kwa ujumla.

Nay wa Mitego ni  moja kati ya wasanii ambao wamezoeleka katika kusema mambo mengi ya watu katika muziki wake. Jambo hili limeweza kumpa umaarufu mkubwa.

Ni mara moja ambayo Nay wa Mitego aliweza kupata changamoto katika muziki wake pale ambapo alikumbana na kisiki cha Nikki Mbishi. Ambapo Nay wa Mitego aliweza kupata ugumu juu ya kujibu chochote kwa Nikki Mbishi maana katika uhalisia Nay Wa Mitego hana uwezo wa midondoko wala uandishi mbele ya Nikki Mbishi.

Hivyo vita hii Nay alilazimika kuizima kimya kimya bila maneno mengi kama alivyozoeleka.

Ila Nikki Mbishi alimaliza vita hii ya kimuziki kwa kuachia wimbo ambao uliitwa  Neema wa mitego, ambapo wimbo huu ulijaa tungo zilizojaa uzito huku midondoko ikiongeza ukubwa wa wimbo huo.

Wimbo huu wa Neema wa mitego ni moja kati ya “DisTrack”bora  kwenye muziki wa kizazi kipya, kwa maana ya wakati wote.

Tumeona sasa Nay amekuwa na maneno mengi katika mitandao ya kijamii husasani mtandao wa Instagram,  lakini pia wimbo wake wa moto ameongea mengi yahusuyo wasanii wenzake kama ilivyo desturi yake.

Ni wazi sasa ameonekana kuanza kumsakama msanii Godzilla, Nay alianza katika wimbo wake wa Moto lakini sasa katika mitandao ya kijamii.

Ila mara zote “mtaka shari si mwepu” kwa maana yule apandaye shari hana maana wala jinsi ya kukwepa shari hiyo bali kuifanya.

Katika hili la Godzilla hatuwezi kumsifu Nay wa Mitego bali kuona ya kuwa ni msanii ambaye ametazama mteremko juu ya mtu mwepesi wa kumsukuma.

Ni wazi kwa sasa Godzilla amechoka kimawazo na upepo wa mtengo mzuri juu ya wale rafiki zake wa Media umekuwa mkubwa. Hivyo Nay hapaswi kulazimisha kumuamsha Godzilla maana usingizi wake wa kimuziki hauwezi kuwa changamoto kwake.

Ila Nay atapata changamoto njema katika muziki ilihali kama atagusa wale nyota waliopo sio yule ambaye yutaabani katika muziki.

Jambo hili la Nay kusema juu ya Godzilla kila lililobaya wala halipaswi kuwa ufahari juu yake, kwa maana ya Godzilla amepoteza fahamu kimuziki.

Nay anapaswa ajitafakari na atazame wasanii walioko sawa kwa sasa ndiyo azungumze awezavyo, kwa maana huwezi kushindana na kitu kisichosema.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa