Ujumbe wa wazi kwa wasanii wote.

Ujumbe wa wazi kwa wasanii wote.

Hakika ni uhalisi yakuwa “Ukijua upande huu basi upande huu hujui” semi hii ni uhalisi wa maisha ya msanii na sanaa yake ya muziki katika usawia wa ujuzi wa kimtandao wenye faida.

Nguvu ya mtandao ni kubwa katika biashara ya muziki, lakini faida indani ya wasanii wachache, hasa wa kizazi hiki cha sasa.

Kizazi cha zamani katika bongo fleva/hiphop kilifanya kazi kubwa mno ambayo malipo yalikuwa ni katika shoo na album. Lakini sasa kuna malipo hata katika ngazi ya mtandao,na leo tutazungumza zaidi kuhusu ‘Youtube’.

Ambapo watu wengi wamekuwa wakila ulaji mzuri kwa kazi za wasanii wengi wa zamani bila haya, huku msanii husika akihaha katika njaa. Kwetu ni chukizo kubwa maana twapenda kila mtu ale kwa haki yake na jasho lake.

Leo hii watu wameweza kuweka nyimbo za wasanii wengi wa zamani ‘Youtube’ huku wakikusanya mapato kila iitwapo siku kwa kuweza kupata watazamaji. Lakini katika pato hilo msanii husika hana ambacho anapata katika ule ukweli. (Fedheha).

Sasa katika ile yenye uwazi na ukweli tunatoa nafasi kwa msanii yoyote yule ambaye anahitaji kuweza kufanya kusanyo la nyimbo zake na kuweka katika mtandao wa ‘youtube’ ili walau apate pato lake katika usasa.

Lakini hata kwa wasanii wa sasa ambao hawajaweza kuweza kupata fedha kupitia ‘Youtube” basi pia tuko wazi katika kumsaidia hilo. Na mswahili hunena yakuwa “Bora kitu kuliko kukosa kitu”

Amka msanii nyimbo husikilizwa/hutizamwa kila leo katika mtandao wa ‘Youtube’ nasi tutayari kukusaidia katika kufaidika na kazi yako. Na amini twasema “Muziki ni biashara isiyo na muda”

Barua pepe tizneez@gmail.com Simu 255-719 476 068

#TuzungumzeMuziki