Ujumbe wa wazi kwa Afande Sele, Watangazaji na Waandishi ‘’Ama kweli! Utu busara,ujinga hasara’’

Afande-Sele-nzuri_full

Ujumbe wa wazi kwa Afande Sele, Watangazaji na Waandishi ‘’Ama kweli! Utu busara,ujinga hasara’’

Kumekuwa na hoja nyingi juu ya wimbo wa Darasa, wimbo ambao sasa umekuwa wimbo wa taifa kwa maana ya rika zote zinacheza na kuimba wimbo huo ambao unaitwa Muziki.

Hoja hizi zimegusa hisia ya wadau na mashabiki wa hiphop. Na haikuwa kificho kujitokeza hadharani kupinga hoja za kusema Darasa ni msanii bora wa hiphop, tena kupitia wimbo wake huu wa Muziki.

Lakini mpaka sasa hakuna msanii wa hiphop ambaye anapinga juu ya uwezo wa ‘kurap’kwa msanii Darasa. Isipokuwa ni chukizo kwao kusema yeye ni bora kwenye utamaduni wa hiphop

Wapo waandishi na watangazaji ambao wamepotosha/wanapotosha watu wakisema wimbo huu ni wimbo wa hiphop. Sina hakika na uwezo wao juu ya ufahamu wao wa muziki wa hiphop. Ukitizama kwa undani utaona jinsi wanavyotumia nafasi zao katika kupotosha kundi kubwa la mashabiki ambalo halijui kuchanganua na kujua kuwa wimbo huu sio wa hiphop.’ Bora kujikwaa kidole kuliko ulimi’

Hili lilitokea hata kwa wimbo wa Og wa Gnako, ambao nao watangazaji na waandishi walisema wimbo huo ni wimbo wa hiphop llihali haukuwa hivyo. Nafikiri wengi wao wakiona msanii ‘amerap’ basi hujua ni hiphop.

‘’Asiyejua maana usimwambie maana’’ hatupaswi kutumia msemo huo katika kujenga kesho zenye uelewa juu ya muziki wa hiphop na muziki mwingine.

Kwanza lazima wajue kuna tofauti kati ya ‘Rap’ na ‘hiphop’ . Sio kila msanii anae ‘rap’ anafanya ‘hiphop’

Kuna mitindo ya ‘Rap’ inayopatikana katika sanaa ya utamaduni wa  ya ‘hiphop’. Hivyo sio kila anaefanya ‘rap’ anawakilisha utamaduni wa ‘hiphop’. Jambo hili lina mifano mingi mno,  Banza Stone(Marehemu)alikuwa anarap na Kitokololo Kuku anarap je tunaweza sema hawa ni wasanii wa hiphop?

Nani anasema mdundo haunamati katika kufanya muziki wa hiphop? Mdundo una nafasi kubwa maana ni desturi ya muziki wa hiphop.

‘’Ama kweli!!hekima haipimwi kwa umri’’ Ni mshangao mkubwa kwa msanii wa hiphop tena mwenye taji la Ufalme wa Rhymes nae akiunga mkono hoja ya watangazaji na waandishi wachache wasiojua tofauti ya muziki wa hiphop, kusema Darasa ni bora kwenye hiphop.

Tena hakuacha kusema vibaya juu ya wasanii wa hiphop ambao huuza Mixtape zao kila leo katika vilinge vya hiphop.

‘’Kwenye miti hakuna wajenzi’’ msemo huu unaenda sawa na maisha ya kimuziki ya Afande Sele.

Ni kweli Afande Sele, watangazaji wameshindwa kujua wimbo wa Darasa ‘’Muziki’’…….. ‘’Utu busara ujinga hasara’’

Itaendeleaa

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Tuachie maoni yako hapa