Uhaba wa tuzo huenda ni kikwazo cha kutokuwa na wasanii wengi wanaowakilisha Tz kimataifa

awards

Uhaba wa tuzo huenda ni kikwazo cha kutokuwa na wasanii wengi wanaowakilisha Tz kimataifa

NA JOHN SIMWANZA

Tanzania ni miongoni mwa nchi za afrika yenye wasanii wengi na kadri siku zinavozidi vipaji vipya vinaibuka lakini cha kushangaza vipaji hivi havifiki mbali hapa namaanisha kuvuka mipaka na kusikika nje ya Tanzania menejiment za ndani nazo ni chache ukilinganisha na idadi ya wasanii tulio nao hatimae wazo la kila msanii linaishia kusimamiwa na menejimenti kama ya Babu tale na mkubwa fella sababu hao ndio wana kiu ya kuwavusha wasanii wetu kimataifa.

Tukizungumzia tuzo hapa tunaweza kufananisha na daraja lingine kabisa la kumvusha msanii katika mipaka ya nje nasema hiyo kwa sababu tuzo huwa inaonesha impact ya msanii ndani ni kwa kiasi gani anakubarika na kuwafanya wasanii wa nje kutamani kufanya nae kazi ili kujitengenezea soko hapa nchini na yeye kumtengenezea soko nchini kwao unapofikia wakati wa tuzo woote tunatambua vyombo vya habari vya ndani na nje huwa vinaelekeza macho yao ili kuhakikisha  wanaripoti kila tukio kwa kila msanii.

Katika nchi yetu tunauhaba wa tuzo kwani tunatuzo kubwa moja tu ambayo imedumu kwa miaka takribani 17 tangu zilipo anzishwa mwaka 1999 na baraza la sanaa Tanzania (BASATA) na kudhaminiwa na kampuni ya vinywaji ya kilimanjaro  mwaka 2003 na kuanza kujulikana kama ‘Kilimajaro Tanzania Music Award (KTMA) tuzo hizi zimejitaidi sana kuwapa heshima na kuwatambulisha wasanii wetu  katika mataifa mbalimbali hasa ya Afrika.

Kungekua na tuzo kubwa zingine sizani kama Msanii wa muziki na Filamu nchini H baba angechukua jukumu la kuandaa tuzo zake binafsi hayo yanajitokeza kutokana na mtu kutopewa heshima yake anayostaili na kuamua kujifariji yeye mwenyewe
Pia hongera Tuzo za Watu ambazo zikipewa nguvu na wadau mbalimbali nazo zitasababisha kukua kwa muziki wetu.

Nchi kama Afrika kusini na Nigeria wasanii wao ndio wanaolitazami soko la marekani kwa sasa na ndio zenye wasanii wengi wanaojulikana kimataifa sio kutokana na kuwa na menejimenti nzuri au lebal kubwa hata wingi watuzo nchini mwao ambazo zinakua zinafanyika mara kwa mara zina wasaidia kusogea mbele na kutambulika zaidi duniani kote hizi ni baadhi ya tuzo  zilizopo Nigeria NEA,KORA,HEADIES na NMVA na Afrika kusini kuna tuzo kama MTVAMA,CHOAMVA,SAMAs, na AFRICAN ARCHIEVER AWARD
Ninaweza kusema kuwa hizi ni vitu wanavyojivunia sana wasanii wa izi nchi mbili katika kujitangaza kimataifa.

Vyombo vya habari ndio tunaviona kwa asilimia kubwa zaidi vikiandaa tuzo mbalimbali duniani kote na hapa nchini ingekuwa ni fursa  kwa vyombo vya habari kuwa na tuzo ili kuukuza muziki na media nyingi hapa  bongo zime base katika Entertainment sasa kwanini vishindwe kuandaa tuzo.

Kwa sababu hiyo ni wazi kabisa uhaba wa tuzo Tanzania ni kikwazo cha kutokuwa na wawakilishi wengi kimataifa endapo tungekua na tuzo kubwa angalau hata nne(4) leo hii tunge waona watanzania wengi sana wakilitafuta soko la dunia katika muziki na kutokana na vipaji vingi navya kuvutia tulivonavyo hapana shaka Nigeria na Afrika kusini wangekua wanafata nyuma yetu.

Makala hii haijaandikwa na Team tizneez, pia tunapokea makala za wachambuzi wengine na kuwapa nafasi hapa katika Category ya Makala. Unaweza kututumia hapa tizneez@gmail.com

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez