“Ugomvi wa fimbo hauamuliwi kwa panga” Diamond Platnumz na Ali Kiba

“Ugomvi wa fimbo hauamuliwi kwa panga” Diamond Platnumz na Ali Kiba

Kila mtu amekuwa akisema lile ambalo limejaza moyo wake kuanzia ngazi ya shabiki, mdau, na hata watu wa Media kwa kile ambacho kinaendelea sasa kati ya Diamond na Kiba.

Lakini uhalisia upo kwa wasanii wawili ambao mara zote wamekuwa wakikanusha kuwa hawana tatizo lolote.

Ila katika uhalisia na ile kweli yenye kweli ni wazi ukweli hujitenga na uongo. Na ni wazi hii imejihidhilisha jana na leo kwa kila mmoja baina ya Daimond na Ali Kiba kutupiana vijembe kwenye mitandao, lakini hii ni baada ya wimbo wa Fresh Remix wa Fid Q akiwa na Daimond lakini Rayvany.

Katika wimbo huo Daimond alitumia fasihi vyema pale ambapo alitupa maneno ambayo yameonekana ni wazi yamemlenga Ali Kiba.

Na mapema tu Ali Kiba alitumia mtandao wa Twitter kuandika machache ambayo katika ile wazi yalikuwa yanaenda kwa Diamond Platnumz.

Hoja ni nyingi kati ya wale ambao wametaka vita hii iishe. Ila ni nani mwenye nguvu ya ushawishi ili vijana hawa waweze kuketi kiti kimoja?

Jambo hili ni gumu mno kama mfano wa paka kuishi chumba kimoja na panya. Kwa upana hawa ni wafanya biashara katika soko moja hivyo mashindano lazima yawepo kila iitwapo leo.

Na njia pekee ya ushindi ni mmoja kutambua mteja anataka nini Zaidi, sio kuishi kwa mazoea Zaidi.

Lakini waugwana yafaa tujue “Wakati wa hari watu hugombea kisima kimoja” Na haya hatuachi kuyasema kwa maana hekima za wahenga zasema “Ukiona neno, usiposema neno, hakutapatikana neno”

Ugomvi huu ni mkubwa mno ndani ya biashara kwa maana ya muziki lakini hata katika maisha ya kawaida. Ni wazi hakuna njia ya nyingine ya kumaliza ugomvi huu Zaidi ya ushindani wa biashara yao.

Kwa maana ugomvi huu ulianza vyema kwenye muziki sio nje ya muziki, na jamii yafaa ifahamu vyema yakuwa “Ugomvi wa fimbo hauamuliwi kwa panga”

Hivyo hata hoja ya kusema mdau Fulani awaite na awapatinishe haiwezi kuwa msaada. Ila njia pekee ni kila mmoja kufanya kazi iliyobora ambayo itakuwa kiushindani kibiashara.

Katika muziki hali kama hizi ni hali za kawaida mno, na daima hufanya kila mmoja atende vyema katika kazi yake ya muziki.

“Penye udhia ndipo penye rupia”

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa