Ufinyu wa mawazo ni kumpa lawama Diamond Platnumz juu ya Aslay na Ali Kiba.

Ufinyu wa mawazo ni kumpa lawama Diamond Platnumz juu ya Aslay na Ali Kiba.

Imekuwa ni chekesho kuu kwa baadhi ya watu kuleta lawama yakuwa “Diamond Platnumz ametoa wimbo kwa lengo la kuvuruga wimbo wa Bembea wa Aslay na Kiba. (Shangazo)

Kimsingi hoja hiyo wasemayo baadhi ya mashabiki na wadaku wakuu ni yenye udhaifu mkuu. (Soni)

Ikumbukwe huu ni muziki na kila mmoja anatoa kwa namna atakayo kwa nyakati zozote zile. Kwani baada ya Aslay na Kiba kutoa wimbo wasanii wangapi nao wakatoa? (Ulizo)

Je! hao walitoa kwa kuvuruga usikivu wa Aslay na Kiba? Hebu watu wawaze kikubwa na kimaendeleo ya muziki. Ni ajabu watu kuwazi kikuda na ufinyu wa upeo. (Ufahamu)

Na uhalisia ni kwamba hakuna msanii ambaye anaweza kuvuruga usikivu wa msanii fulani bali hofu ni tawala tu. (Uoga)

Na kama baadhi ya watu wanaamini yakuwa Diamond ametoa wimbo huo kuvuruga usikivu wa Aslay na Kiba, basi ni vyema tukubaliane yakuwa hakuna kama Diamond sasa. (Eeh)

Kwa maana akitoa tu watu wanahamia kwake, sasa watu huwa wanapinga nini? Lakini ni vyema kuwaza kibiashara yakuwa mtu hawezi kuacha kuweka bidhaa sokoni kisa fulani kaweka. (Hakika)

Kila mtu aweke bidhaa yenye ubora na namna ya ubunifu kamili, ushindani wenye tija huleta hamasa ya muziki na mafanikio kamili. (Uhalisia)

Kwanini watu baadhi wawe na uoga juu ya wimbo huu wa Yope? Ikumbukwe wimbo huu ni wa Yope ni mali ya Linnossb na Diamond ni msanii shirikishwa tu. (Ndiyo)

Na tukirejea kwa Aslay na Kiba wao hupata usikivu wa Vyombo vya habari vyote, huku Diamond ni kwa uchache mno, sasa hofu ya kuwazima inatoka wapi? (Ujinga)

Ikumbukwe Aslay na Kiba ni katika kutembelea kabisa vyombo vya habari na kuzungumzia wimbo wao, ilihali Diamond ni mtandaoni tu. (Naam)

Sasa hofu ya kuzimwa yatoka wapi? Uwanja wa muziki ni mpana mno, kila msanii atoe kazi kwa nyakati atakayo. Hakuna wa kumzima mwanzake bali bidhaa yenye ubora kamili. (Hakika)

#MuzikiNiSisi