Uelewa mdogo unawatesa mashabiki wengi kwenye bongo fleva.

240_F_46539406_tB9OHdxAWNyDMrOhEj02PPPlSkn0IXg1

Uelewa mdogo unawatesa mashabiki wengi kwenye bongo fleva.

Sioni tena washabiki kama ilivyokuwa miaka kadhaa nyuma, ila naona watukanaji hodari, hivi ni kweli huwezi kumshabikia mtu mpaka uongeze na matusi?

Si jambo baya kupeana elimu katika mambo mengi mazuri ambayo kimsingi yangejenga zaidi na kuendelea kukuza muziki huu. Lakini imekuwa tofauti kabisa na wengi ambao hujiita mashabiki ambao kiuhalisia siamini kama msanii husika anafurahi kuona mshabiki wake akiwa ni mwenye lugha ya matusi mbele ya mashabiki wengine.

Leo hii imekuwa ni jambo baya hata mtangazaji/mchambuzi akiweka picha ya msanii fulani basi ni matusi juu yake. Na huyo mshabiki anaetukana hujiita balozi wa msanii husika, je balozi anakuwa na matusi? Naamini balozi anakuwa mwenye busara ili aendelea kukusanya mashabiki wengine kupitia yeye.

Nimekuwa msomaji mzuri wa moani katika swala zima ambalo jana lililokuwa likiendelea kwenye tuzo za BET ambazo zimefanyika nchini Marekani.

Diamond Platnumz ni msanii pekee aliyetuwakilsha Afrika ya Mashariki katika tuzo hizo ambapo alikuwa kwenye kipengere cha Best International Act Africa. Na hapa alikuwa akichuana na wakali kama WizKid, Yemilade,Black Coffee, na AKA.

Black Cofee ndiye msanii aliyeibuka mshindi katika tuzo hizi. Na Diamond Platnumz hakusita kumpa hongera kupitia mtandao wa picha “Instagram”

Ni baada ya muda mfupi katika ukurasa wa BET kwenye mtandao wa picha hali ilibadilika na ikawa na lugha kali ya mutusi juu ya picha waliokuwa wememuweka mshindi wa tuzo hizo ambaye ni Black Coffee.

Kiuhalisi ni jambo ambalo linaonyesha ni jinsi gani hakuna mashabiki bali watukanaji katika muziki huu. Jambo pekee ambalo nilijiuliza kwanza hivi kwanini tumekuwa washamba wa mitandao kiasi hichi? Kwanini hatujui kuwa watu wa kushukuru na kujipanga zaidi katika mwaka mwingine?

Wapo ambao walisema pia hawamjui Black Coffee amewezaje kupewa tuzo hiyo huku wakiongeza na matusi. Hili sio jambo jema, ni vyema kujifunza kutumia mtandao wa kijamii vyema, lugha kali haisaidii zaidi ya kuonekana ni jinsi gani uelewa wako ulivyo mdogo.

Lakini pia Black Coffee sio msanii mdogo kama wengi walivyokuwa wakidhihaki katika ile posti ya BET hata katika ukurasa wake pia.

Black Coffee ni msanii na dj wa muda mrefu nchini Afrika ya kusini. Ni moja kati ya wasanii wachache wenye uwezo wa kujaza kiwanja cha mpira katika nchi hiyo. Black Coffee ni miongoni mwa wasanii wenye album nyingi pia ambapo mpaka sasa na album 5.

Album yake kwanza iliitwa Lack Coffee (Soulistic Music, ambapo ilitoka mwaka 2005) pia kufuatiwa na nyingine Have Another One (Soulistic Music, 2007). Lakini hakuishia hapo Album ya Home Brewed Soulistic Music,ilitoka mwaka 2009, na nyingine zilizofuta ni Africa Rising DVD (Soulistic Music, 2012) , Africa Rising CD (Soulistic Music, 2012) na Pieces of Me (Soulistic Music 2015).

Hivyo ukitazama si msanii mdogo kama wengi walivyokuwa wanasema kwa kutumia lugha ya matusi. Ifike mahala tuache tabia kama za lugha ya matusi, ila kama wewe ni mshabiki wa msanii wowote yule ni vyema kujifunza kutumia lugha yenye kuleta amani zaidi sio kuharibu.

Lugha kali ya matusi haijengi, isipokuwa watu kuona ufinyu wa upeo wako ulipoishia. Pia hoja yako itaonekana ya maana zaidi kama hutaweka lugha yenye matusi.

Kuwa balozi mwema wa msanii wako, ili utengeneze mashabiki wengine zaidi.

Team tizneez inakupongeza Diamond Platnumz pia tunaamini wewe ni mshindi wetu wa Afrika ya Mashariki.

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez