Tuwashangae wanaoshangaa wasanii wa hiphop Tanzania kukosa nafasi Afrimma.

Tuwashangae wanaoshangaa wasanii wa hiphop Tanzania kukosa nafasi Afrimma.

Tunaona hoja ni nyingi kwanini kwenye Tuzo za Afrimma hakuna msanii yoyote wa hiphop Tanzania? (Ulizo)

Na wenye kuuliza ni wale wale ambao wanasema hiphop haiuzi wala hailipi. Lakini wenye kuuliza ni wale wale ambao kutwa hupendezwa na udaku mkuu. (Upuuzi)

Wenye kuuliza ni wale wale hata siku moja hakuwahi/hawakuwahi kuweka kazi ya hiphop katika upana wake na kusifia, bali kutwa ni hubiri yakuwa “Hiphop haiuzi” (Ujinga)

Takwimu za hiphop haiuzi wanatoa wapi? Na kama haiuzi mbona wasanii wenye kufanya hiphop kwa mapana wanatoa album na kanda mseto kila leo? (Ajabu)

Ni vyema kuacha unafiki hodari, unahoji/wanahoji kwanini hatupati nafasi katika tuzo nyingi ilihali huna/hawana muda wa kuzungumza wala kutangaza kazi za hiphop katika jana yake bali leo tuzo. (Soni)

Tunawakumbusha tena na tena yakuwa “Huwezi kwenda kwa jirani pasina kutokea kwako”. (Daima)

Kama kutwa wewe huthamini cha kwako jirani atakithamini vipi? Lakini mzunguko wa kucheza muziki wa hiphop haupo je! nje watasikia vipi? (Kabisa)

Wenye kuuliza zaidi kuwa kwanini hatushiriki ni wale katika kurasa zao kutwa ni posti za udaku na fedheha si hiphop. (Eeh)

Sasa hiyo nafasi inakuja kwa namna ipi? walio nje wataona wapi kazi zetu za hiphop?. Kama hiphop ingepewa mzunguko hapa ndani kwa ukubwa ni wazi tungeshiriki kwa mapana. (Hakika)

Na katika uhalisi tuna wasanii wengi na wenye uwezo wa  kufanya hiphop kwa upana wake. Lakini nguvu ya media na kurasa kubwa katika nyakati hizi ni udaku uliomkuu. (Fedheha)

Listi hii katika tuzo hizi za Afrimma ni yenye uwepesi mkuu katika upana wa wasanii wetu. Vivyo kama walio wengi wataendelea kuhubiri udaku ni wazi tusitaraji kushiriki. (Hakika)

Tunaandika haya kwa mapana na ujuzi kwa kuwa tundani ya Hiphop na hakuna kurasa wala blog yoyote Tanzania yenye kuhubiri Hiphop kama Tizneez. (Iko Wazi)

Na tunawakumbusha tena yakuwa “Mshale usio na nyoya hauendi mbali” Na kivazi cha unafiki katika hoji yakuwa kwanini hatushiriki ni vyema mkivue. (Soni)

Na nguvu kuu ya wengi ni sifu ya Kaligraph Jones kuliko Nikki Mbishi, Ama Sarkodie kuliko Fid Q, lakini hata Phyno kuliko Joh Makin. (Mifano)

Sasa kwa unafiki huo nguvu ya kuhoji mnapata wapi ilihali kutwa ni kunena yakuwa “Hiphop haiuzi” na wale ni bora kuliko wetu, sasa leo kutoshiriki katika tuzo shangazo lenu ni lipi? nyakati mlishasema haiuzi na wale ni bora? (Unafiki)

Tukiipa nguvu hiphop na kuweza kupata mzunguko ni wazi tutashiriki vyema kwenye tuzo ila kufanya matamasha katika nchi nyingi za nje. (Matangazo)

Na daima “Mwenye akili hujenga nyumbani, bali mpumbavu ugenini. (Sifu)

#MuzikiNiSisi 

www.tizneez.com