Tuwashangae wanafiki wanaomshangaa Ray C (Shangazo)

Tuwashangae wanafiki wanaomshangaa Ray C (Shangazo)

Mwanzo wake ni katika ubora wa hali ya juu lakini heshima yake ilikuwa ni katika ukubwa wenye ujazo kamili wa msanii mwenye uimbaji na urembo wenye mvuto halisi. (Juzi).

Bomoa la heshima yake lijuu yake yeye mwenyewe si mwingine, changanyo la mengi katika ujanja wa umaarufu na ulevi wake hakika ni anguko kamili. (Jana)

Endelezo ni katika kujikongoja zaidi na mbuga ya muziki ni kubwa mno na ongezeko la wanyama wengi katika uzao unafanya wenye mbunga yao kuishi kwa shida kubwa. (Ndiyo)

Lakini wenye mbuga yao na wenye upana wa maarifa wameendelea kuwepo kwa uhakika wa juu huku wakifanya makubwa mbele ya wanyama wapya huku wapya wakibaki na ushangazo. (Lady Jaydee).

Koo la Ray bado zima katika uimbaji hakika amathibitisha kwenye wimbo wake na Kaligraph Jones ambao waitwa Unanidatisha uliotoka mwaka jana 2018 mwezi wa 6. (Hakika).

Lakini Rogaroga (2018.10) ukazidi kudhihilisha yakuwa kipaji cha uhakika hakiwezi kupotea hata iweje. Na wajuzi ni wenye Imani kubwa juu ya Ray C katika usawia wa uimbaji wa kileo.

Ni wazi licha ya rudi imara katika mbuga ya muziki hakuweza kupata muda wa kutosha katika vyombo vya habari. (Kweli).

Na wapo wapuuzi kadhaa wananena eti!alikuwa Kenya ndiyo maana hakupata hata mahojiano juu ya nyimbo hizo au kuzicheza kwa upana. Kwani Davido yuko Tanzania? Mbona nyimbo zake zachezwa kwa ukubwa?. (Ajabu)

Dunia ya leo mtu anaweza kufanyiwa mahojiano au wimbo wake kuchezwa hata awe wapi. (Uhalisia)

Sisi hatushangazi Ray C kutingisha wowowo lake katika uwazi kabisa kiasi cha kutamani hata kutoa nguo alizovaa katika mtandao wa picha “Instagram” maana ni wazi ametaka mahojiano lakini kuzungumziwa kwa upana. (Eeh)

Kwani hatuoni mahojiano mengi wanapewa zaidi wenye hovyo nyingi za mtandao? Sasa tunashangazwa nini na Ray C? ina maana hamuoni wenye hovyo wanavyopata mengi ya faida kwa maana ya pato mara tu wafanyapo ya hovyo?

Basi tusishangazwe na Ray hata kwa udogo bali kusifu maana “Mpe mjinga sifa yake ili asipate uelevu” naam. Ni wazi mashabiki mmepewa mnachotaka vyema.

Maana katika uhalisi hata ukirejea katika posti za nyimbo zake hazikuwa na maoni mengi toka kwa mashabiki, lakini posti ya kutingisha wowowo imepata maoni mengi zaidi.

Hii inadhihilisha wajinga na wapenda hovyo wako wengi kwa uwingi, lakini kama vyombo vya habari vikiweka mbele ‘Elimu burudani’ hakika puuzi hizi zitaisha kwa upana.

Na daima “Kheri mrama kuliko kuzama” Umri wa Ray C hapaswi kwenda na upepo wa mtandao hata kidogo bali tulizo la kazi zenye katika msingi imara zaidi. (Naam)

Lakini msisahau semi ya mswahili yakuwa “Maji yaenda njia yake” (Ufahamu)

#MuzikiNiSisi