“Tuwashangae ambao wanawashangaa akina Gigy Money wapya”

“Tuwashangae ambao wanawashangaa akina Gigy Money wapya”

Kauli ya muziki una mambo mengi ni kauli kubwa ambayo huenda ambaye hajui kuhusu mengi ya muziki asielewe.

Hatuachi kusema kila baya lenye kuharibu muziki huu mzuri wa kizazi kipya ambao mwanzo wake ulikuwa umejaa wasanii waliowekeza kwenye kipaji lakini wengi wa sasa kwenye mwili Zaidi.

Lakini haitushangazi sisi kwa maana tunajua “Usipoumiza akili kwa hakika utaumiza mwili”

Na tunaona kwa upana wadada ambavyo wanaumiza miili ya ili tu kuweza kuingia vyema kwenye muziki, maana sasa kuingia kwenye muziki si kipaji tena ila mambo yasiyofaa Zaidi uyatende vyema ili uingie kirahisi kwenye ramani ya muziki.

Kila kukuchapo tunaona kwa upana wakina Giy Money wapya wakiibuka na kufanya Zaidi ya ajabu kuliko vile ambavyo walifanya/wanafanya aina ya wadada kama Gigy Money.

Wanafanya haya kwa kuona namna ambavyo sasa wale ambao walifanya yakipuuzi kupewa nafasi kubwa kwenye Media na kuona kama wameweza kutimiza malengo yao.

Na hili liko wazi wengi wenye mambo ya hovyo hupewa nafasi kubwa, lakini vipaji vya ukweli kunyimwa nafasi.

Hatuwezi kufumba vinywa vyetu kusema hili, wapo wasemao yakuwa “Kuwazungumzia ni kuwapa nafasi maana utakuwa umetimiza lengo lao” lakini lazima mjue bila kuisema chungu hii haiwezi kuisha hivyo tunakila sababu ya kusema.

Na leo hii wapo (Media) ambazo zinashangaa kuongeza kwa kina Gigy money wengi ilihali hao ndiyo walikuwa wachonga vyema barabara juu ya kuzungumzia mengi ya kipuuzi na sio muziki.

Hivyo wakati mzuri ndiyo huu ni vyema #TuzungumzeMuziki na sio kingine kwa maana mengine hayana msingi wala maana katika maisha ya Sanaa yetu.

Ila pia yapasa mjue “Chema chajiuza kibaya chajitembeza” na matokeo ya hawa kina Gigy Money wapya ni mbegu waliyopanda wao wenyewe. (Media)

#TuzungumzeMuziki.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa

 

 

 

 

Attachment