Tusilazimishane kuhuzunika wala kufurahi kila mmoja abaki na lake alilolichagua. (Lady Jaydee)

Tusilazimishane kuhuzunika wala kufurahi kila mmoja abaki na lake alilolichagua. (Lady Jaydee)

Ni wazi kwa jamii za waswahili ni muhimu mno kuwa muungwana kwa upana. Lakini uungwana ni zao la tulivyotendeana awali kati na mwisho. (Hakika)

Ni jamii hii ya waswahili (Tanzania) tumeshuhudia Punda akiombewa kheri kuliko mtu. Tena si mtu ilimradi bali kiongozi wa Serikali. (Ajabu)

Kwa maana hiyo watu waliamua kufanya maombi kwaajili ya punda, je! wangepingwa? (Hapana) yale ni katika amuzi lao. (Ndiyo)

Kwa maana hiyo basi hatupaswi kupangiana cha kufanya katika lolote bali katika uamuzi la mtu ndani yake. (Eeh)

Ni shangazo kuona watu pia wanamlazimisha dada mkuu Jide kuweka posti ama kusema lolote juu msiba wa Ruge. (Shangazo)

Unajua ifike mahala watu wajitambue, Hivi Jide asiposema lolote inabadilisha nini? Kwaiyo Jide ni muhimu kuliko Serikali nzima? au muhimu kuliko watanzania waliojitoa kusimama barabarani katika jua kali ilimradi kupunga tu mkono? (Upuuzi)

Jide aachwe na alichokichagua kwa maana ndicho alichokichagua, hatupaswi wala haipaiswi eti kulaumu lolote kutoka kwake. (Uhalisia)

Unalaumu nini juu yake? maana ndicho alichokichagua, pia unajua ameumia kuhusu msiba ama? (Hatujui) 

Tunadhani hekima si kulaumu watu bali hekima ni kuhubiri kweli na mema ya Ruge katika wengi zaidi, tukianza kunyoosheana vidole yakuwa huyu kaposti huyu hajaposti hakika ni upuuzi. (Unafiki)

Ingawaje kwa waswahili sisi “Msiba humaliza tofauti, lakini nyakati nyingine msiba huongeza tofauti” (Yote)

Na rudio la kweli yenye kweli ni “Tusilazimishane kuhuzunika wala kufurahi, kila mmoja abaki na alichokichagua”  (Uamuzi)

#MuzikiNiSisi