Tusiishie kumpongeza Chege ila afanywe chanzo bora.

Tusiishie kumpongeza Chege ila afanywe chanzo bora.

Siri ya mafanikio ni kujiamini wakati wote. Wakati wasanii wengi wakiendelea kuhuburi yakuwa album haiuzi lakini wenye sauti kali kwenye media kusema haina faida kabisa ni wazi tumepoteza vyema uwanja wa album katika muziki wa kizazi kipya.

Na jambo hili limefanya http://tizneez.com/makala/wasanii-wengi-wa-bongo-bado-chipukizi-kwa-kukosa-album/

Team Tizneez tuliwahi kuandika http://tizneez.com/makala/tafakari-kuu-ya-kukosa-album-kwenye-muziki-kizazi-kipya/

Lakini katika andiko hilo tulisema “Tatizo halikimbiwi bali kutafuta njia bora za kulipunguza kama sio kuliondoa kabisa”

Ni wazi kwa Chege kutoa album yake sasa ameonyesha ushujaa mkubwa, na haipaswi kuishia kupongezwa kwenye mitandao ya kijamii wala media lakini atumike kueleza namna ambavyo ataweza kuuza na ameweza kuuza

Na tunaamini kupitia yeye tunaweza kurudisha vyema soko zima la album kwenye muziki wetu ambapo sasa una ulemavu wa album.

Album ya Chege inaitwa RunTown na ina nyimbo 14 na album hii inapatikana katika ngazi zote za mtandao.

Hivyo mashabiki huu ndiyo muda wa kumpa ushirikiano Chege katika kufanya apate faida ya album yake.

Shabiki sema #MimiSitumiWimboWhatsApp Msanii sema #ShabikiUsitumeWimboWhatsApp #TumaLinkWhatsApp

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa