Tusichanganye ya mwanzo, kati na mwisho katika kifo cha msanii na Media.

Tusichanganye ya mwanzo, kati na mwisho katika kifo cha msanii na Media.

Daima kuna mwanzo, kati na mwisho katika uisho wetu, lakini changanyo la wengi ni katikati na daima husahau kabisa kuhusu mwanzo. (Eeh)

Mwisho huwa ni katika lawama kubwa, ilihali mwanzo ni katika mapendo ya hali ya juu, na ndiyo maisha yalivyo. (Naam)

Tumeona mwisho za wasani wengi mno ni katika lawama nzito hasa pale Media inapoamua kutoa muda wa heshima kwa msanii fariki. (Uhalisi)

Wengi huona kama ni dhihaka, huku wengine wakienda mbali wakinena yakuwa “Media zinafanya kosa kucheza muziki kwa ukubwa mara msanii akifariki”.

Ni wazi Media haifanyi kosa hata kidogo bali kuonyesha heshima na kuthamini kazi na mchango wa msanii husika katika uwanja wa Sanaa. (Kabisa)

Na jambo hili si Tanzania pekee bali mfumo wa Dunia, msanii anapofariki muziki wake huchezwa kwa mapana makubwa. Na hata zile tovuti ambazo huuza muziki pia huuza sana kazi zake. (Uhalisi)

Sasa kipi ambacho kinashangaza kwetu kiasi cha mashabiki na wasanii kadhaa  kutupa lawama kwa Media? (Shangazo)

Na wenye kulalama katika hili je!wewe uliwahi kufanya hilo kwa msanii gani/yupi katika kumpa heshima?

Hakuna shida kwa Media kucheza nyimbo na hata watu wengine kuweka hisia zao katika mitandao, yote ni katika heshima kubwa ya msanii husika. (Thamani)

Ikumbukwe mwanzo hauwezi kuwa sawa na kati kwa maana nyakati, leo huwezi kusikia mzunguko mkubwa wa nyimbo za msanii kama Afande Sele shauri ya nyakati. (Ndiyo)

Wasanii wenye kutoa shutuma kwa Media ni vyema mtafakari kwa makini mno kabla hamjafungua vinywa vyenu maana yake mnatia aibu kubwa. (Soni)

 

#MuzikiNiSisi