‘Tunapaswa tubadilike kulingana na mazingira, ila sio kila mazingira yatubadilishe’Maalum kwa Dayna Nyange.

‘Tunapaswa tubadilike kulingana na mazingira, ila sio kila mazingira yatubadilishe’Maalum kwa Dayna Nyange.

“Daima shahidi ndiye mwenye neno” hainipi tabu juu ya kumfahamu Dayna Nyange ambaye ni mwanamuziki wa Bongo fleva ambaye miaka 7 nyuma ndipo alipotambulika kwenye ramani ya muziki wa kizazi kipya na wimbo wake wa ‘mafungu ya nyanya’ ambao alimshirikisha Marlaw.

Wakati Dayna anachipuka na kutambulika haikuwa kazi ngumu kwake maana hakika ni moja kati ya wasanii wa kike wachache ambaye aliweza kuja na umimi wake. Ni wazi wasanii wengi wa kike walikuwa ni waigaji wazuri wa kila kitu kutoka kwa wasanii wa kike wakubwa kwa wakati ule.

Zipo nyimbo nyingi ambazo amewahi kutoa Dayna Nyange na zikafanya vizuri, ila Nivute kwako ni miongoni mwa nyimbo zake ambazo zilidhihilisha ubora wake zaidi kuwa si msanii wa kubahatisha bali kipaji chake cha hali ya juu.

Mkusanyo wa mashabiki katika muziki wake uliendelea kupanda siku baada ya siku kupitia nyimbo kama, Angejua, Komela na nyingine nyingi.

Ila jamii ikumbuke tangu kufahamika kwa Dayna Nyange miaka kadhaa nyuma hakuwa msanii aliyefahamika kwa mambo ya kipuuzi bali muziki wake.

Ni wazi mwaka 2016 ndio mwaka bora zaidi katika maisha ya kisanii kwa upande wa Dayna Nyange. Maana ameweza kuwa mdomoni mwa mashabiki wengi wa muziki wa kizazi kipya. Yote ni shauri ya muziki wake ambao mara zote hutoa bila kujali nani ametoa wimbo gani wakati huo.

“Ukienda mbio na muda mtapishana” Ni moja kati ya misemo ambayo tunapaswa kuipa nafasi katika maisha ya kila leo.

Lakini pia “Huwezi kuona msitu ukiwa msituni” Kauli hii inaenda sawa na maisha ya Dayna Nyange ambayo anaishi sasa katika muziki wake. Ni wazi Dayna haoni kama anakosea kuwa nusu uchi mbele ya mashabiki wake hasa kwenye mtandao wa picha ‘Instagram’, lakini anapaswa kujua wakati anaingia kwenye muziki na kuweza kupata mashabiki hakuwa anajiweka wazi kiasi hichi cha sasa. Mashabiki walijali muziki wake zaidi, sio kujiweka nusu uchi kama afanyavyo sasa.

“Tunapaswa tubadilike kulingana na maziingira, ila sio kila mazingira yatubadilishe”

Ukitazama maisha ya muziki ya Dayna Nyange ni wazi  mazingira yamembadilisha wa kiwango kikubwa. Ila mazingira ambayo ameweza kwenda nayo ni ya kuwa nusu uchi zaidi, ambapo kimsingi haijengi jina lake ila  kubomoa.

Dayna anatumia kasi kubwa ya kutengeneza jina kwa ubaya huku akidhani ameshindwa kutengeneza jina kwa uzuri. Maana katika media nyingi tumeona jinsi ambavyo wale ambao walitengeneza jina kwa ubaya wanavyopewa nafasi huenda jambo hili linafanya Dayna kubadilika na mazingira hayo.

Ila mimi ni moja ya wachache ambao naamini katika kipaji cha Dayna Nyange, ni vyema kuachana na kasi ya upepo ya umaarufu wa wadada wengi usio na maana (Nusu Uchi).

Hivyo haina maana ya yeye kutumia nguvu kubwa ya kuwavuta mashabiki wake kupitia mwili wake, ila akitumia nguvu kubwa kupitia muziki ni jambo jema analopaswa kulifanya wakati wote.

Ni vyema yale ya kiki za mitandaoni kuwaachia wahusika ambao hawana heshima yoyote mbele ya jamii, simamia zaidi muziki wako.

Ikamate kauli hii wakati wote ““Tunapaswa tubadilike kulingana na maziingira, ila sio kila mazingira yatubadilishe”

Lakini usifuate kauli hii ‘Ukishindwa kutengeneza jina kwa uzuri tengeneza kwa ubaya’ Dayna Nyange.

 

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa