Tuna mashabiki wengi wa matukio na sio muziki. (Hakika)

Tuna mashabiki wengi wa matukio na sio muziki. (Hakika)

Mtu mwenye kupenda na kufuatilia kwa undani kitu ama jambo na kulipa nguvu ni wazi huyo ndiye shabiki. (Uhalisia)

Na nyakati hizi si kama za awali ambapo wengi wao ilikuwa furaha yao ni ujazo wa wimbo mzuri wenye tungo imara. (Muziki)

Sasa hizi ni nyakati za ushabiki wa matukio na ujazo wa soni kuu kuliko muziki wenye uimara na maana kuu. (Fedheha)

Nyakati za soni ya ugomvi wa Tid na jamaa ambaye sisi hatukuwahi kumjua ilikuwa ni shangwe ya wengi katika furaha yenye hovyo. (Soni)

Na kilichofuata ni jamaa kupewa mahojiano mengi mno, ambapo kimsingi haikuwa na maana yoyote. (Ajabu)

Dhihaka ikawa tawala kwa Tid ambaye ni wazi ukitaja wasanii wenye upana wa kuchangia kukua na kuenea ni mjinga pekee anaweza asitaje jina lake. (Naam)

Leo yake ni wimbo wake wa Any More akiwa na Lady Jaydee. Ambapo ni wimbo wenye ujazo wa tungo, uimbaji na mdudo. (Muziki)

Lakini ile nguvu iliyotumika na Media na mashabiki katika sambaza ya matukio yake haipo katika sambazo ya wimbo wake huu. (Ujinga)

Hii inatuonyesha wazi kuwa tuna mashabiki wengi wa matukio kuliko muziki wenyewe. Hili si jambo jema kabisa. (Hakika)

Lakini tuchukue nafasi kumpongeza Tid kwa wimbo mzuri na bora. Ni wazi zimetoka nyingi mno, lakini Any More na Tid ni yenye ujazo wa wimbo wenye usikivu mkuu nyakati zote. (Ubora)

#MuzikiNiSisi