Tumesoma andiko Ray Vany kuhusu wimbo Mwanza imetupa mashaka (Sikitiko)

Tumesoma andiko Ray Vany kuhusu wimbo Mwanza imetupa mashaka (Sikitiko)

Maana ya Sanaa ameelezea vyema katika mgandamizo mzuri toka mtandaoni (Ndiyo)

Lakini ametuacha hoi mno katika semi ya kuwa wimbo huu ni zawadi kwa watu Mwanza katika upana wa faraja baada ya Mv Nyerere kuzama. (Ajabu hii)

Hivi kweli wimbo huu unaweza kuwa zawadi ya faraja? (Ujinga)

Unamlenga nani katika zawadi hii? kikundi cha washenzi wenye hovyo zaidi? (Ulizo/Shangazo)

Au unalenga wote ambao walioguswa na ajali ile kwa maana ya watoto na watu wazima? (Tujuze)

Tunajua yakuwa unataka nguvu ya kujitetea katika hili lakini koseo lipo katika wimbo. Na kweli itatuweka huru zaidi. (Kosa)

Usifanye masikhara katika kunena wimbo ulikuwa lengo la faraja kwa ajali, hakika usijaribu kuweka ongo yako ifanane na ukweli. (Pumbavu)

Wimbo wa faraja hubeba zaidi jumbe yenye uhalisi katika nyakati kamili, hii jumbe ya faraja ipi zaidi? upana wa neno ‘Nyege’ katika rudio ndiyo faraja? semi za Amber Ruty ndo faraja ya Mv Nyerere? (Jamani)

Huu haukuwa wimbo wa faraja usijaribu kutupanga watu wenye ujazo kamili wa tafakari. Bali tungo nyepesi zenye shenzi kubwa. (Eeh)

Ivae aibu yako katika tungo nyepesi zenye uwazi wa lugha kali, usitake kuitupilia mbali aibu hii. (Ichukue)

Sanaa ni uburudishaji lakini sanaa pia ni elimishaji, kwa hili umeburudisha mno. (Kweli). ila swali la msingi kama ulijua wimbo huu unaachiwa kwa watu wa miaka 18 na kuendelea uliweka angalizo? (Swali)

Mbona uliachia bila angalizo, na furaha ilitawala katika namna ya wimbo unavyotembea, sasa unataka kutupanga nini? (Tafakari)

Ni vyema unene mengine lakini swala la faraja ya ajali ya Mv Nyerere uliache kama lilivyo, hakuna wimbo wa faraja Duniani wenye mfanano tofauti na ajali husika. (Hakika)

Kweli ukubwa wa msiba ule wa Mv Nyerere upate faraja kwa wimbo huu? hee! haya ni maajabu ya Dunia katika uhalisi huu. (Nishai)

Ni vyema ukachutama na kuomba radhi pia kwa ongo ya faraja katika upana wa ajali ya Mv Nyerere. (Fikiria)

Na daima “Huwezi kuona msitu ukiwa msituni” sisi wajuzi huwezi kutuzuga kwa kucheza na lugha ya sanaa wala lugha ya sheria, hili liko wazi, ni ngumu kubadili maana hii mithili ya nyekundu kuwa njano. (Hakika)

Sanaa itumike vyema, kukiwa na nyimbo/wimbo ni vyema kuwe na angalizo jema zaidi. (Uhalisi) 

Ray Vany tafakari na uandike tena yenye ujazo wa hoja, kwa hii ni hoja nyepesi mithili ya pepo za bahari ya hindi. 

Na kama uongozi umeruhusu uje na hoja hii hakika unatupa uhalisi wa “Kipofu hawezi kumuongiza kipofu mwenzake, wote wataanguka shimoni” Tafakuri zaidi)

#TuzungumzeMuziki