Tukumbuke kumbukumbu juu ya Bi Kidude

Tukumbuke kumbukumbu juu ya Bi Kidude

Bibi kidude ni nguli wa muziki afrika, na jina lake halisi ni Fatuma Binti Baraka.

Ingawaje hakuna kumbukumbu ya uhalisi wa mwaka wake wa kuzaliwa. Na wakati alipofariki 17/4/2013 inakisiwa alikuwa na miaka 102.

Na hata nyakati za uhai wake hakuwahi kujua alizaliwa tarehe, mwezi wala mwaka bali kusema alizaliwa wakati rupia ikitumika kama fedha.

Tukikumbuka kumbukumbu ni wazi Bi Kidude alizaliwa katika kijiji cha Mfagimarigo visiwani Zanzibar, katika familia ya watoto saba.

Bi kidude ni mjuzi wa utunzi na uimbaji wa muziki wa Taarabu. Muziki ambao asili yake ni arabuni lakini una vionjo vya mwambao wa pwani kama Lamu, Mombasa. Zanzibar, Bagamoyo na Tanga.

Na alianza kuimba akiwa na umri wa miaka 10, na chanzo kikuu cha uimbaji wake ni msanii Sitti Bint Saad.

Licha ya utunzi na uimbaji lakini Bi Kidude alikuwa ni mfanyabiashara wa Hina na Wanja lakini tabibu wa miti shamba ilihali hata uwalimu wa Unyago.

Muhogo wa Jangombe ni wimbo ambao ulimpa umaarufu zaidi katika nchi nyingi kama Ufaransa, Oman, Hispania, Ufilipino, Ujerumani na Uingereza.

Lakini Bi Kidude ni msanii ambaye alikuwa anaweza imba kwa kutumia lugha mbili Kiswahili na Kiarabu. Ilihali hana elimu ambayo aliwahi kupata zaidi ya Kurani.

Lakini katika uhalisi wa ujuzi wa muziki kuwa hauzeeki wala haushi bali baada ya maisha ya kifo, Bi Kidude aliweza kushiriki katika muziki wa kizazi kipya.

Na wasanii ambao walipata bahati kuweza kushirikiana nae katika kumbukumbu ya maktaba yetu ni wawili tu.

Ambapo ni kundi la Offside Trick na wimbo waitwa Ahmada.

Wakati Fid Q akiwa msanii wa pili na wimbo waitwa Juhudi za wasiojiweza.

Hakika Bi Kidude sasa anaishi katika kifo, maana “hata kufa ni kuishi ilihali ni katika kifo”

Nasi twasema Maisha mema katika maisha ya kifo.

Ilhali waswahili wamazoea sema “Pumzika kwa Amani”

#TuzungumzeMuziki