“Tuhamie Mwezini”Ukweli ulionyimwa nafasi.

 

1350873579_RAMA_DEE___Rama Dee Katika picha juu

“Tuhamie mwezini “ya Danny Msimamo, Suma G na Rama Dee ukweli ulionyimwa nafasi

Kuna wakati inabidi turudi kutazama yaliyopta ili tujifunze yaliyomema katika maisha yetu ya mbele, tuache ule msemo usemao” kilichopita kimepita”vipo vilivyopita vyenye maana kila iitwapo leo.

Ni miaka miwili imepita tangu kutoka kwa wimbo wa Tuhamie Mwezini wa msanii Dany Msimamo ambaye sasa pia ni mjumbe wa Shirikisho la Muziki Tanzania (SHIMUTA), wimbo wa tuhamie mwezini alimshirikisha Rama Dee na Suma G. Ambapo wimbo huu ulitoka 2014

danny-msimamo

Danny Msimamo katika picha juu.

“Kwenye vituo vya radio hakuna muziki mzuri”hii ni kauli ambayo hupenda kuisema rafiki yangu Steven Ole Moruo, ambayo kiukweli ilinipa shida kuikubali,lakini baadae hata mimi kuanza kuamini kuwa muziki mzuri haupo radioni, yani katika vituo vya radio.

Kipenda Roho ya Rama Dee imenifanya niamini tena na tena kuwa Radioni hakuna muziki mzuri. Huu ni wimbo mpya wa Rama Dee ambapo kabla ya wimbo huu kulikuwepo na Usihofie Wachaga. Usihofie Wachaga ni wimbo wake uliosikika mwaka jana (2015) ambao pia hakupewa nafasi katika vituo vya radio, vile ambavyo ilistahili.

Zipo nyimbo nyingi nzuri tu ambazo hakika hazijapewa nafasi hata kidogo katika media zetu hapa Tanzania. Ila tumeona zipo nyimbo nyingi ambazo hupewa nafasi lakini katika uhalisia si nyimbo nzuri, isipokuwa ni urafiki, ubinafsi, rushwa, kutopenda ukweli, kumefanya nyimbo hizo mbovu kupewa muda mzuri katika vituo vya radio na runinga, na hatimaye kuonekana ni bora kwa wasikilizaji walio wengi. Ila ikumbukwe lazima waone bora maana ndicho wanachokisikia katika muda huo.

Hakika hakukuwa na sababu za msingi ya wimbo huu wa Tuhamie Mwezini kutokuchezwa katika vituo vya radio hasa vile ambavyo ilistahili. Tuhamie mwezini ni wimbo ulizungumza yaliyomema ambayo ilipaswa kila mpenda muziki wa kizazi kipya apate kupata elimu iliyotolewa humo.

“Wenyewe hatupendani nani atatupenda”moja kati hoja zilizosemwa katika wimbo huu wa Tuhamie Mwezini. Kiuhalisia ni msemo ambao unaingia katika maisha yetu ya kila siku, ila kwa hapa wacha nizungumzie zaidi kuhusu muziki wa kizazi kipya. Hivi unajua kweli hakuna upendo kati ya msanii, mtangazaji, dj na hata mdau? Cha ajabu wote wanaunganishwa na kitu kimoja muziki.

Tuhamie Mwezini ulikuwa ni wimbo mkubwa na bado ni wimbo mkubwa. Hakika aina ya nyimbo hizi zenye maisha marefu ni kitu tulichokosa sasa katika miaka hii hasa kwenye muziki wetu wa kizazi kipya.

index

Suma katika picha juu

Wimbo huu ulipata kuwa na kila kitu ambacho wimbo wowote mzuri lazima uwe nacho. Ujumbe ni kitu cha kwanza, hakika hutaweza kupinga ujumbe ambao ulitolewa katika wimbo huu. Ni wazi waligusa maisha ya mtanzania anayoishi kila siku iendayo kwa Mungu. Mdundo ni moja wapo kati ya kinogesho cha wimbo huu, mdundo wake ni wazi utakufanya utikise kichwa huku ukiendelea kupata ujumbe wenye kukujuza mengi yenye faida katika maisha yako ya kila siku.

Huwezi kuutaja wimbo huu bila kutaja ukubwa wa kiitikio alichofanya mkali wa Rnb Tanzania Rama Dee, ambaye ameweza kuutendea haki wimbo kuanzia mwanzo mpaka mwisho. Hakika uzuri wa sauti yake umefanya wimbo kuwa bora zaidi. Suma G ndiye msanii aliyekamilisha verse ya tatu katika wimbo huu, maana verse ya kwanza na ya pili imefanywa na mmiliki wa wimbo huu Dany Msimamo.

Utofauti wa Suma G yule wa vituko uswahilini ulionekana wazi katika wimbo huu.“Nyumba yangu wamebomoa wajenge uzio wa wanyama, Biashara yangu wamebomoa kisa ujio wa Obama” Hoja kadhaa alizosema Suma G. Ni wazi alikuwa tofauti na vile tulivyomzoea, na hapa alionyesha maana halisi ya msanii anavyotakiwa kuwa.

Wimbo huu unanipa hoja nyingi za kutafakiri hata kuzungumza. Kuna haja ya kupunguza chuki, ubinafsi, rushwa, umkoa, katika vituo vya radio ambavyo ni wazi wasikizaji wake wanakosa kujua nyimbo nzuri ambazo ni wazi walipaswa kujua kupitia hizo radio wanazosikiliza kila iitwapo leo

Ni kweli tuna tofautiana mawazo, daima hatuwezi kuwa na mawazo sawa ila yapo mengine yanayonekana katika uwazi mkubwa. Hivyo ni vyema kujifunza kuweka wazi ili kusaidia wengi wasiojua nini ni nini.

Isikilize hapa Tuhamie Mwezini ya Danny Msimamo Feat Rama Dee $Suma G

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez