Tofauti ya wakazi na wasanii wengi tofauti.

Tofauti ya wakazi na wasanii wengi tofauti.

Ukizungumza juu Album mbele ya mashabiki, wadau au wasaniii wa Bongo Fleva/Hiphop majibu ya walio wengi watakujibu Album hazilipi, Album haiuzi au Album ni biashara ya muziki wa zamani.

Lakini Album ina umuhimu mkubwa katika kujenga maisha ya sanaa ya msanii husika. Kupitia album msanii atajiweka heshima itakayo mfanya msanii asipotee katika midomo ya wadau wa muziki lakini vizazi na vizazi ambavyo vitahitaji kujua kuhusu muziki.

Licha ya hoja dhaifu ya album haiuzi msanii Wakazi ameamua kwenda tofauti na hoja hiyo na tofauti ya wasanii wengine wengi.

Wakazi sasa yupo mbioni kuachia album yake ya ‘Kisimani’. Jambo hili ni jema na kupongezwa maana wasanii wengi wameamini Zaidi ile hoja dhaifu ya album haiuzi ilihali hawana uhakika.

Ila hakuna sababu za kushangaa msanii akiamini hoja dhaifu ya mauzo ya album, kwa maana “Mjinga husadiki kila neno”

Album ya Wakazi itauza kama tu media zitamua kumpa muda uliobora katika kutangaza vyema album yake hiyo. Ila kasumba tuliyonayo watanzania wengi ni kuthamini Zaidi mambo ya nje kuliko yetu. (Ushamba)

Nguvu iliyotumika kuzungumzia album ya Jay Z ikitumika kuzungumzia album ya Wakazi kisimani hakika atauza kwa maana wakati wote biashara ni matangazo. Ila watu wa media walio wengi wako radhi kuzungumzia kiki za wasanii ambazo kimsingi hazina faida wala maana katika kuendeleza muziki mbele. Hii ndiyo maana ya Tizneez kuanza kampeni ya #ZimaKikiWashaMuziki.

Utofauti ambao amethubutu kufanya wakazi una kila sababu ya kupewa muda ili tuweze kurudisha soko la album katika muziki wetu wa kizazi kipya.

Kama team Tizneez tuna kila sababu ya kupongeza jitihada za namna hii ili kuweza kusonga mbele kimuziki.

 

#KisimaniAlbum

 

#ZimaKikiWashaMuziki.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Tuachie maoni yako hapa