Tofauti ya ufanyaji muziki sasa na uhalisi tofauti wa Belle 9.

Tofauti ya ufanyaji muziki sasa na uhalisi tofauti wa Belle 9.

Na wajuzi wanaamini yakuwa kujua tofauti ya ‘jinsi na ‘kuwa’ ndiyo ngao imara ya Belle 9 katika kila leo kwenye muziki wake.

Maana katika kweli yenye kweli wasanii wengi hawajui “jinsi” ya Sanaa ya muziki katika ufanyaji bali usimamio imara wa matendo nje ya muziki yenye fedheha. (kiki)

Na katika uhalisi hakuna heshima juu ya wasanii wenye kiki kuliko muziki wenyewe mbele ya wajuzi wa muziki na wenye kusimamia mtazamo wa #TuzungumzeMuziki, na hakika #ZimaKikiWashaMuziki.

Bali fedheha ni tawala katika mioyo ya wajuzi wenye ujuzi wa muziki, lakini kwa wasiojua maana ya “jinsi”ya Sanaa muziki hakika wao ni sawia tu kila jambo. (Soni).

Lakini Belle 9 amejua vyema ‘jinsi’ ya Sanaa ya muziki itakavyo kwa maana ni kusimamia Sanaa yenyewe sio egemeo la kiki. Ingawa katika uhalisia changamoto ni kubwa maana wapotoshaji ni wengi katika simamio imara la mengi yenye upuuzi.

Hivyo yataka msanii ajue undani wa ‘jinsi’ ya Sanaa ya muziki ili asipepee na upepo wa kiki ambao hauna maana bali udhalilishaji tu.

Ila kujua ‘kuwa’ Sanaa ya muziki ni kuifanya kwa uwezo wake wa kuimba katika simamio ya kwamba muziki ni hisia kunafanya Belle 9 abaki kuwa yeye na ubora wake katika nyakati zote.

Na mswahili anena yakuwa “Hekima ni kuzuia miguu yako kufuata hovyo” naam yapasa Belle 9 abaki katika njia yake kuu ya muziki tu.

Na katika uhalisi wajinga wasipoona ujinga pia hupenda kilichopo katika nyakati hizo, hakika ‘dada’ ni moja ya wimbo bora katika nyakati hizi na zijazo, mdundo, uimbaji, na mashairi kwa hakika tunapaswa tuseme.

#TuzungumzeMuziki.