Tofauti ya maana katika ‘neno’ kifungo halali cha Ray Vany na Diamond Platnumz.

Tofauti ya maana katika ‘neno’ kifungo halali cha Ray Vany na Diamond Platnumz.

Msingi wa neno katika uhalisi ni sehemu fupi ya lugha yenye ujazo wa maana. Ila pili ni sauti yenye kunenwa au kuchapishwa na kutaja jambo fulani. (Hakika)

Lakini kwa mfumo wa ‘neno’ kuna nyakati huwa fupi au refu katika ‘Mofimu’ (Sauti yenye uwakilishi wa maana fulani).

Vivyo kwa ukawaida ‘neno’ ni kusanyo la ‘silabi’ kadhaa zikiwemo ‘konsonati’ na ‘vokali’. (Uhalisi).

Wajuzi wa lugha daima hutofautiana katika aina za maneno kwa upana wa Nomino, Kitenzi, kihisishi, kivumishi, kiunganishi, kielezi, na kiwakilishi.

Katika pana la wimbo wa Ray Vany na Diamond hakika maana ya neno tajwa mara nyingi halileti maana katika wengi, hakika limejaa soni. (Naam)

Tuanze na neno ‘Nyegezi’ hili neno lenye ukamili, na upana wa lugha kwenye neno linasimama kama ‘Nomino’. (Fahamu)

Lakini urudio wa neno ‘Nyege’ unaleta maana tofauti ya katika ufikirio mpana. Na ni vyema tusijitie upofu katika shabikio bali tafakari yenye maana. (Hakika)

Neno’Nyege’ linasimama katika uhalisi wa ‘kitenzi’ ama ‘kielezi’ na kwa maana hiyo linakuwa neno lenye kujitegemea. (Uhalisi)

Je! kuna kosa katika kufungia wimbo huu? hakika kwa wajuzi hakuna katika upana wa neno kwa maneno yenye urudio zaidi. (Ndiyo).

Lakini ni vyema mfumo wa Basata ubadilike katika utendaji kazi maana leo hii katika mtangazo wa kifungo cha wimbo huu unafanya wimbo kuzidi songa mbele zaidi. (Hakika)

Na hii ni kiki kubwa kwa Wasafi,  hakika ufungio wa wimbo huu watautumia vyema katika kukikisha zaidi na zaidi.(Naam)

Yote ya yote wimbo una mitambao mizuri mno, lakini mdundo wa Black toka Ostrich Music unaleta ladha tofauti juu ya Wasafi. Lakini changanyo la Laizer la uchanganyi unakamilisha usikivu imara.

Hivyo utumizi wa lugha ya sanaa katika uwazi unakamilisha kifungo kamili cha wimbo huu. (Naam)

Na mswahili hunena yakuwa “Shika shika lingali kichwani” Tafakarii…….

www.tizneez.com kusoma zaidi fuata kiunga kwenye ukurasa wetu juu.

#TuzungumzeMuziki